Dollar

41,8473

0.04 %

Euro

48,7208

0.28 %

Gram Gold

5.647,1600

1.4 %

Quarter Gold

9.570,2800

2.24 %

Silver

71,2500

2.92 %

Hata hivyo, ACT Wazalendo imesisitiza kuwa itachukua hatua zaidi dhidi ya maamuzi hayo, ikiwemo kukata rufaa na kuwashirikisha wadau mbalimbali, ndani na nje ya nchi.

Safari ya Luhaga Mpina kuwania Urais wa Tanzania yafikia mwisho

Karata ya mwisho ya mgombea urais wa Chama cha ACT Wazalendo imekwama baada ya Mahakama Kuu, Masjala Kuu Dodoma kumuondoa rasmi Luhaga Joelson Mpina kwenye kinyang'anyiro hicho kwa madai kwamba hoja zilizo wasilishwa hazikuwa na mashiko.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na chama cha ACT Wazalendo, Oktoba 15, 2025, Mahakama Kuu ya Tanzania (Masjala Kuu) Dodoma, imekubaliana na hoja za serikali na kuliondoa shauri la chama hicho mbele ya Mahakama hiyo.

Hata hivyo, ACT Wazalendo imesisitiza kuwa itachukua hatua zaidi dhidi ya maamuzi hayo, ikiwemo kukata rufaa na kuwashirikisha wadau mbalimbali, ndani na nje ya nchi.

Katika uamuzi huo wa kurasa 32 Mahakama imeamua kuwa Luhaga Joelson Mpina hawezi kuendelea na mchakato wa kampeni za kuwania nafasi ya Urais kupitia tiketi ya chama cha ACT Wazalendo.

“Tunasikitika kuwataarifu kuwa Mahakama Kuu imekubaliana na hoja za serikali na hivyo kuliondoa shauri letu mbele ya Mahakama,” taarifa hiyo imesema.

Hukumu hiyo hapo awali ilipangwa kutolewa tarehe 10 mwezi huu lakini Mahakama ilisita kutoa na kuomba muda wa nyingeza ili kuamua hukumu kwa haki.

Shauri hilo la kikatiba namba 24027 la mwaka 2025 lililofunguiliwa na aliyekuwa mgombea urais wa Chama Cha ACT Wazalendo luhaga Mpina lilisikilizwa kwa njia ya mtandao.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#