Sport
Dollar
41,8375
0.03 %Euro
48,6825
0.16 %Gram Gold
5.627,9400
1.05 %Quarter Gold
9.360,7700
0 %Silver
70,1400
1.33 %Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na makundi ya waasi, yakiwemo waasi wa M23, wamesaini makubaliano mjini Doha ya kuanzisha utaratibu wa kufuatilia utekelezaji wa usitishaji mapigano, serikali ya Kongo imetangaza Jumanne.
DRC na makundi ya waasi, yakiwemo AFC/M23, walisaini makubaliano hayo Jumanne mjini Doha ili kuweka mfumo wa ufuatiliaji wa usitishaji mapigano, ikiwa ni juhudi za hivi karibuni kumaliza machafuko mashariki mwa DRC.
Hafla ya utiaji saini ilifanyika chini ya uangalizi wa nchi ya Qatar, ambayo ndiyo nchi mpatanishi, na ilishuhudiwa na wawakilishi waangalizi kutoka Marekani, Umoja wa Afrika, na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO).
"Wajumbe kutoka DR Congo na River Alliance/M23 walisaini Jumanne mfumo wa ufuatiliaji na uthibitishaji wa usitishaji mapigano, chini ya uangalizi wa Qatar," Wizara ya Mawasiliano ya DRC ilisema kupitia ujumbe kwenye mtandao wa kijamii X.
Pande hizo zilitia saini makubaliano ya kanuni za kusitisha mapigano huko Doha mwezi Julai.
Hatua kubwa
Hata hivyo mapigano yanaendelea kati ya vikosi vya serikali na waasi wa M23, huku kila upande ukishutumu mwingine kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano.
Serikali ilisema makubaliano ya Jumanne ni hatua kubwa katika utekelezaji wa kanuni za tamko zilizotiwa saini mnamo Julai 19.
Kwa kusainiwa makubaliano hayo, DRC "inathibitisha nia yake ya kufikia usitishaji wa vita, kudhamini usalama wa watu, na kuandaa mazingira ya makubaliano ya amani ya kudumu, ndani ya mfumo wa mchakato wa Doha unaoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa," wizara hiyo ilisema.
M23 inaelezea mpango huo kama 'hatua kubwa'
Kundi hilo linadhibiti eneo kubwa, ikiwa ni pamoja na miji mikuu ya majimbo ya Goma na Bukavu, baada ya kuyateka mapema mwaka huu.
Umoja wa Mataifa, Kinshasa na wengine wanaishutumu nchi jirani ya Rwanda kwa kuunga mkono M23, jambo ambalo Kigali inakanusha.
Waasi wa M23 walielezea mpango huo wa Jumanne kama hatua kubwa.
Comments
No comments Yet
Comment