Dollar

43,1997

0.03 %

Euro

50,3204

0 %

Gram Gold

6.409,9900

-0.32 %

Quarter Gold

10.585,2500

-0.23 %

Silver

128,1300

-1.07 %

Makubaliano hayo yanatoa fursa kwa Kenya kupeleka asilimia 98.2 ya bidhaa zao katika soko la China bila kutozwa ushuru.

Kenya yafikia makubaliano ya awali ya 'kutotoza ushuru'  bidhaa na China: wizara

Kenya imefikia makubaliano ya kibiashara na China ambayo yataruhusu Kenya kupeleka asilimia 98.2 ya bidhaa zake katika soko la China bila kulipia ushuru, wizara yake ya biashara ilisema siku ya Alhamisi, ikiongeza kuwa pande hizo mbili zimekuwa zikifanya majadiliano katika kutafuta mkataba wa biashara wa mataifa yote mawiili.

Taifa hilo la Afrika Mashariki limekuwa na uhusiano wa karibu na China, huku Rais William Ruto akifanya ziara rasmi ya kitaifa nchini China mwaka uliopita, ambapo makubaliano kadhaa ya kifedha na ya ushirikiano yalitiwa saini.

"Tumeanzisha majadiliano na China kuzungumzia makubaliano ya mataifa yetu mawili ya biashara," wizara ya biashara ya Kenya ilisema katika taarifa, ikizungumzia kuhusu mazungumzo hayo kwa mara ya kwanza. "Mazungumzo haya yametufikisha katika hatua ya makubaliano ya awali."

Ruto ametetea kuwa na uhusiano mzuri na China dhidi ya shutma kutoka kwa maafisa wa Marekani, akisema lazima iuze bidhaa nyingi katika soko la Asia ili kupunguza hali ya kutokuwa sawa ambapo inaonekana China inafaidika zaidi.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#