Dollar

0,0000

%

Euro

0,0000

%

Gram Gold

0,0000

%

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Serikali ya Uganda imetangaza rasmi tarehe 15 na 16 Januari 2026 kuwa siku za mapumziko ili kutoa fursa kwa raia ya kushiriki kwa ukamilifu katika zoezi la kupiga kura

Uganda inasema iko tayari kwa uchaguzi mkuu

Zaidi ya wananachi milioni 21.6 wa Uganda wako tayari kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Januari 15.

Wananchi hao kazi yao kubwa itakuwa kuchagua viongozi wao kutoka ngazi ya urais, wabunge na hata viongozi wa serikali za mtaa.

Kuna jumla ya wagombea 8 wanao wania nafasi ya urais, akiwemo Rais aliye madarakani Yoweri Museveni ambapo atakuwa anaomba ridhaa ya kuongoza nchi hiyo kwa awamu ya saba.

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo idadi ya wapiga kura waliojiandikisha katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu ni kubwa kuliko ile ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2021 ambapo zaidi ya wapiga kura milioni 18.1 walijiandikisha.

Serikali ya Uganda imetangaza rasmi tarehe 15 na 16 Januari 2026 kuwa siku za mapumziko ili kutoa fursa kwa raia ya kushiriki kwa ukamilifu katika zoezi la kupiga kura.

Nchi hiyo ya Afrika Mashariki hata hivyo, itapiga kura bila raia wake kuwa na huduma ya intaneti. 

Hii ni kwa mujibu wa Tume ya Mawasiliano ya Uganda kutangaza kusimamishwa kwa huduma ya mtandao pamoja na uuzaji mpya wa kadi za simu kuanzia jioni ya tarehe 13 Januari 2026.

Tume ya Mawasiliano imesema, hatua hiyo ni katika jitihada za kupunguza kuenea kwa kasi kwa taarifa potofu mitandaoni zinazohusiana na uchaguzi.

Tayari hatua hiyo ya serikali imepata ukosoaji mkubwa, hasa kutoka kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu na vyama vya upinzani, wakisema hiyo itaathiri uwazi wa upigaji kura na kutolewa kwa matokeo ya uchaguzi.

Wakati huo huo, mbali na kukata mtandao, serikali pia imeamuru mashirika mawili ya haki za mitaa ambayo yamekuwa yakikosoa mamlaka kusitisha kazi zao.Mashirikia hayo ni Chapter Four Uganda and Human Rights Network for Journalists-Uganda.

Kwa upande wake, waangalizi kutoka Umoja wa Afrika na mashirika mengine kama COMESA, IGAD na Jumuiya ya Afrika Mashariki tayari wako nchini Uganda kuangalia jinsi zoezi la upigaji kura litakavyokwenda.

Tume ya Uchaguzi imewaonya wapiga kura kutovaa mavazi yenye rangi au ujumbe wa vyama vya kisiasa pindi wanapokwenda kupiga kura.

Chama cha Wanasheria wa Uganda nacho kimesema zaidi ya wanachama wake 600 nchini kote watafuatilia uchaguzi huo kwa karibu.

Kutakuwa na Mfumo wa Uthibitishaji wa Wapigakura kwa kutumia mashine za kielekroniki zikiwa na uwezo wa kuhakiki na kuthibitisha taarifa za wapigakura.

Vifaa vinaweza kufanya kazi kwa muda wa hadi saa 20, ambayo inatosha kushughulikia zoezi zima la upigaji kura.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#