Dollar

43,1591

0.1 %

Euro

50,2889

-0.09 %

Gram Gold

6.372,1100

0.07 %

Quarter Gold

10.547,9300

0.43 %

Silver

120,6300

2.16 %

Mamlaka nchini humo zimewataka wakazi wa maeneo hayo kuwa waangalifu, na kuepuka maeneo yenye mafuriko.

Afrika Kusini yaonya kuwepo kwa mamba na viboko katika maeneo ya makazi baada ya mvua kubwa

Serikali ya Afrika Kusini imewatahadharisha wananchi wake katika mkoa wa Limpopo kuwa waangalifu baada ya wanyama hatari ikiwemo mamba na viboko, kuonekana katika makazi ya watu kufuatia mvua kubwa zilizosababisha mafuriko katika mabwawa na mito.

Huduma ya Hali ya Hewa ya Afrika Kusini (SAWS) siku ya Jumanne imetoa tahadhari ya Kiwango cha 9 na 6 inayotahadharisha kuhusu hali mbaya ya hewa kwa mikoa ya Limpopo, Mpumalanga na Gauteng, ikiwatahadharisha watu dhidi ya mafuriko, barabara kufungwa, maporomoko ya udongo na mawe, huku mvua kubwa zikiendelea.

Mamlaka za mikoa zimesema mamba wameonekana katika makazi ya watu maeneo ya Makuleke na Mhinga, nje ya Malamulele. Mamba wanaaminika kutoka katika mito ya karibu na mabwawa yaliyojaa maji kutokana na mvua zinazoendelea, kwa mujibu wa Shirika la Habari la Taifa SABC.

Maafisa wa mazingira nao wametahadharisha kwamba baadhi ya wanyama wengine wa mwituni, ikiwemo viboko, wanaweza kuonekana baada ya maji kuongezeka, na kuwataka wananchi kuepuka maeneo yenye mafuriko, na kutoa taarifa haraka iwapo watawaona wanyama hao.

Jitihada za uokozi

Hali hiyo mbaya ya hewa pia imehatarisha maisha ya watu. Mamlaka zimethibitisha kukwama kwa mwanamke mmoja na watoto wake wawili katikati mwa Mto Mutale.

Jitihada za kuwaokoa zimekwamishwa na hali mbaya ya hewa.

Godfrey Nefolovhodwe, mkazi wa kijiji cha Gwakwani kilichopo nje ya Thohoyandou, ameiambia ABC mvua kubwa na kuongezeka kwa kiwango cha maji imefanya vikosi vya uokozi kushindwa kuwafikia wale waliokwama.

"Inanyesha sana, maji yako kila mahali ninapozungumza sasa. Watu watatu wamekwama ndani ya Mto Mutale na bado wapo hai," alisema. "Wamekwama huko tangu jana. Kuna baridi, mvua inaendelea, na maji yanaonekana kuongezeka kila dakika. Timu za uokoaji zilikuwepo, lakini zilisema hazitaweza kusaidia kwa sababu hali ni tete sana."

Mamlaka zimewaomba wakazi katika maeneo yaliyoathirika wachukue tahadhari kubwa, kuepuka maeneo yaliyojaa maji, na kufuata ushauri wa usalama wakati huduma za dharura zinaendelea kufuatilia hali na kujiandaa kwa matukio zaidi yanayohusiana na hali ya hewa.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#