Dollar

43,1809

-0.01 %

Euro

50,4337

0.14 %

Gram Gold

6.378,3000

-0.82 %

Quarter Gold

10.609,8100

0 %

Silver

122,4200

-5.48 %

Rwanda imetuma kikosi cha wahandisi wa kijeshi kwenda Jamaica ili “kusaidia juhudi za kujenga upya taifa hilo la Karibi kwa kukarabati miundombinu iliyoharibiwa na kimbunga kikali” mwaka 2025, Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) lilisema Jumatano.

Rwanda yaungana na Ghana katika kutuma wahandisi wa kijeshi nchini Jamaica

Kwa mujibu Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF), kupeleka huko kwa wanajeshi ni baada ya kuwa na makubaliano na nchi ya Rwanda.

“Jambo hili la kupeleka wanajeshi limefanyika kwa mujibu wa makubaliano ya mataifa mawili kati ya Rwanda na Jamaica, yanayolenga kusaidia ukarabati wa miundombinu muhimu iliyoharibiwa na majanga,” ilisema taarifa ya RDF.

Taarifa hiyo rasmi haikubainisha idadi ya wataalamu waliotumwa.

Wahandisi hao wa kijeshi wa Rwanda walipokea maelekezo kutoka kwa Brigedia Jenerali Faustin Tinka, kabla ya kuondoka Kigali kuelekea Jamaica.

‘Utaalamu na weledi’

Brigedia Jenerali Tinka “aliwahimiza wanajeshi waliotumwa kutumia kikamilifu utaalamu wao, weledi, na ujuzi wa kiufundi ili kutekeleza kwa mafanikio jukumu walilokabidhiwa na uongozi wa RDF,” jeshi lilisema katika taarifa yake.

Kimbunga Melissa kilikumba eneo la Karibi mwishoni mwa Oktoba 2025, na kusababisha uharibifu mkubwa.

Jamaica ndiyo iliyoathirika zaidi, hali iliyosababisha vifo vya watu kadhaa na kuchochea juhudi kubwa za misaada ya kibinadamu kutoka taasisi mbalimbali.

Mnamo Disemba, Ghana ilituma wahandisi 54 wa kijeshi kwenda Jamaica kusaidia kujenga upya miundombinu muhimu baada ya kimbunga hicho kusababisha hasara inayokadiriwa kufikia dola bilioni 8.8 za Marekani.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#