Sport
Dollar
42,8044
0.17 %Euro
50,1756
-0.07 %Gram Gold
5.973,2500
0.3 %Quarter Gold
9.852,9100
0.24 %Silver
92,4600
2.85 %Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimiol akuongezea ujumbe wa kulinda amani nchini DRC MONUSCO mwaka mmoja zaidi
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio la kuongeza mamlaka ya wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO kwa muda wa mwaka mmoja.
MONUSCO, mojawapo ya ujumbe wa muda mrefu zaidi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa ulianzishwa mwaka 2010 ili kuendeleza na kupanua juhudi za Umoja wa Mataifa za Kulinda Amani na kuleta utulivu nchini DRC.
Ilipokea mamlaka baada ya kusitishwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Congo Monuc, ambayo ilikuwa kazi tangu Novemba 1999.
Kwa sasa kuna karibu wanajeshi 11,000 na polisi waliotumwa kama sehemu ya operesheni hiyo.
Ukomeshwaji wa FDLR na M23
Wakati huo huo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani mashambulizi ya M23 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na kuitaka Rwanda kuacha kuwaunga mkono waasi na kuondoa wanajeshi wake.
Baraza hilo lenye wanachama 15, pia lilitaka wanajeshi wa Congo kusitisha kuunga mkono makundi kama vile FDLR na kwamba DRC itimize ahadi yake ya "kulipokonya kundi hilo silaha mara moja."
FDLR ilianzishwa na Wahutu waliokimbia Rwanda baada ya kushiriki katika mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 yaliyoua karibu Watutsi milioni moja na Wahutu wenye msimamo wa wastani.
M23 inasema inapigania kulinda jamii za kabila la Watutsi mashariki mwa Congo.
Hatua ya hivi punde ya M23 mashariki mwa Congo yenye utajiri wa madini imekuja wiki moja baada ya Rais wa Congo Felix Tshisekedi na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame kukutana na Rais wa Marekani Donald Trump mjini Washington mapema mwezi huu na kuthibitisha kujitolea kwao kwa mapatano ya amani yaliyosimamiwa na Marekani.
Rwanda, ambayo inasema wanajeshi wake wako mashariki mwa Congo kwa kile inachoita hatua za kujihami, imekanusha madai ya kuunga mkono M23 na imevilaumu vikosi vya Congo na Burundi kwa kuongezeka kwa ghasia za hivi punde.
Comments
No comments Yet
Comment