Sport
Dollar
42,7934
0.13 %Euro
50,2152
-0.02 %Gram Gold
5.976,6200
0.35 %Quarter Gold
9.852,9100
0.24 %Silver
92,3700
2.76 %Shirika la Umoja wa Mataifa linasema raia wanakimbia wakiwa na hofu huku mapigano yakienea kote katika miji muhimu katika maeneo ya Kordofan ya Sudan
Watu zaidi ya 50,000 wamekuwa wakimbizi wapya tangu mwishoni mwa mwezi Oktoba huku mapigano yakikithiri, Shirika la Kimataifa la Wahamiaji (IOM) lilionya siku ya Ijumaa, likisema raia raia wanakimbia kwa hofu siyo kwa kupenda kwao.
"Watu nchini hawaondoki kwa kupenda, wanakimbia kwa ajili ya usalama," alisema Mohamed Refaat, mkuu wa Shirika la IOM nchini Sudan, akizungumza na waandishi wa habari walioko Geneva kutoka Port Sudan.
Refaat alisema wanaoondoka katika makazi yao Kordofan ni kutokana na kuongezeka kwa vita, huku wakazi wakikimbia kutoka miji ikiwemo Babanousa, Kadugli na El-Obeid.
Alizungumzia ripoti za wapiganaji wa RSF pamoja na washirika wao wa Sudan People's Liberation Movement-North kushambulia majengo ya makazi ya watu katika maeneo ya Dilling, Kordofan Kusini, katika kipindi cha saa 48 iliopita.
Wanawake na watoto
RSF imekuwa ikipigana na jeshi la Sudan tangu Aprili 2023, kufuatia kusamvaratika kwa utawala wa mpito wa kiraia. Oktoba 26, vikosi vya RSF vilivamia Al Fasher, mji mkuu wa Darfur Kaskazini, baada ya kuwafungia watu kwa siku 500, kusababisha watu wengi kuondoka katika makazi yao na wengine kukwama wakiwa hawana chakula.
Refaat alisema kuwa wengi ya wale wanaokimbia ni wanawake na watoto, hasa wale wanaowasili kutoka majimbo ya White Nile na Gedaref.
Pia alionya kuhusu hali mbaya eneo la Kadugli, ambapo ndege zisizokuwa na rubani zilishambulia wiki iliopita na kuwaua walinda amani sita kutoka Bangladesh walio na vikosi vya Umoja wa Mataifa huko Abyei.
Kama mapigano yataendelea, "tunakadiria watu 90,000 hadi 100,000 wanaweza kuwa bila makazi yao" kutoka Kadugli pekee, alisema, akiongeza kuwa El-Obeid inaweza kuwa "hatua moja au mbili" kwa mashambulizi kama hayo, pengine kuathiri watu zaidi ya nusu milioni.
Afisa wa IOM pia alionya kuwa kupunguwa kwa ufadhili kumefadhili shirika hilo kupunguza shughuli zake, likisema limepoteza dola milioni $83 mwaka huu.
"Inabidi tuchague maisha gani tunataka kuokoa," alisema, akitoa wito kwa mataifa kuongeza juhudi za misaada kwa raia wa Sudan.
Comments
No comments Yet
Comment