Sport
Dollar
0,0000
%Euro
0,0000
%Gram Gold
0,0000
%Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Shambulio la droni la RSF limeua walinda amani sita kutoka Bangladesh na wengine wanane kujeruhiwa, tarehe 13 Disemba.
Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha Mpito cha Abyei (UNISFA) kilitangaza Alhamisi kuwa kimehamisha kambi yake ya vifaa kutoka mji wa Kadugli, jimbo la Kordofan Kusini nchini Sudan, kufuatia shambulio hatari lililolenga walinda amani wake.
Tarehe 13 Desemba, walinda amani sita kutoka Bangladesh waliuawa na wengine wanane kujeruhiwa baada ya shambulio la droni lililotekelezwa na kikosi cha kijeshi cha RSF. Shambulio hilo lililenga makao makuu ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa mjini Kadugli.
Hata hivyo, UNISFA ilisisitiza kuwa bado itaendelea kutekeleza wajibu wake katika eneo hilo na inaendelea kufuatilia kwa karibu hali inavyoendelea. Iliongeza kuwa itazingatia kurejea na kuanza tena shughuli zake mjini Kadugli pale hali ya usalama itakaporuhusu.
UNISFA ilipelekwa katika eneo hilo mwaka 2011 baada ya mvutano kuongezeka kati ya Sudan na Sudan Kusini kuhusu eneo lenye utajiri wa mafuta.
Kwa mujibu wa mashirika ya kutetea haki za binadamu, mji wa Kadugli umekuwa chini ya mzingiro uliowekwa na RSF pamoja na washirika wao wa Sudan People’s Liberation Movement-North (SPLM-N) tangu miezi ya mwanzo ya vita, na umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara kwa makombora na droni.
Vita kati ya jeshi la Sudan na RSF, vilivyoanza Aprili 2023, vimesababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwafanya mamilioni ya wengine kuyahama makazi yao.
Comments
No comments Yet
Comment