Sport
Dollar
42,7973
0.11 %Euro
50,2861
-0.04 %Gram Gold
5.955,9600
0.01 %Quarter Gold
9.828,8400
0 %Silver
90,0600
0.19 %Shirika la Umoja wa Mataifa linaloratibu uhamiaji limerekodi matukio 39 ambayo yamesababisha watu kuondoka kwenya makazi yao kutoka eneo la Kordofan tangu Oktoba 25
Raia zaidi ya 50,000 wameondoka katika makazi yao kwenye majimbo matatu huko Kordofan kusini mwa Sudan kwa sababu ya kuongezeka kwa ukosefu wa usalama, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) lilisema Alhamisi.
Shirika hilo la Umoja wa Mataifa linasema jumla ya watu 50,445 walikimbia kutoka kwa eneo la Kordofan kati ya Oktoba 25 na Disemba 17 huku ukosefu wa usalama ukikithiri.
IOM inasema maafisa wake wanaofuatilia watu walioondoka katika makazi yao wamesajili matukio 39 ambayo yalisababisha idadi kubwa ya watu walioondoka katika makazi yao kutoka eneo hilo tangu Oktoba 25.
Shirika hilo lilieleza kuwa watu karibu 40,350 waliondoka katika makazi yao kutoka maeneo sita Kaskazini mwa Kordofan, watu 9,845 kutoka maeneo tisa Kusini mwa Kordofan na 250 kutoka Magharibi mwa Kordofan.
Mamlaka za Sudan, Umoja wa Mataifa, na mashirika ya haki za binadamu ya eneo hilo na kimataifa yameshtumu wapiganaji wa RSF kwa ukiukwaji wa haki za binadamu na ubakaji katika miji kadhaa ya eneo hilo.
Kundi hilo la waasi limekanusha kuwalenga raia, ingawa wakati mwingine wanakiri kuwepo kwa “ukiukwaji” Darfur na kudai kuanzisha uchunguzi kwa ukiukwaji wa haki za binadamu.
Kati ya majimbo 18 ya Sudan, RSF inadhibiti majimBo yote matano eneo la Darfur magharibi mwa nchi, isipokuwa kwa baadhi ya maeneo kaskazini upande wa Kaskazini mwa Darfur ambayo yanadhibitiwa na jeshi. Jeshi, nalo, linadhibiti maeneo mengi ya majimbo 13 yaliyobakia kusini, kaskazini, mashariki, na katikati, ikiwemo mji mkuu, Khartoum.
Mapigano kati ya jeshi la Sudan na RSF, yaliyoanza Aprili 2023, yamesababisha vifo vya maelfu ya watu na kufanya mamilioni wengine kuondoka katika makazi yao.
Comments
No comments Yet
Comment