Sport
Dollar
42,7408
0.04 %Euro
50,2033
0.02 %Gram Gold
5.944,7300
-0.31 %Quarter Gold
9.801,8200
-0.24 %Silver
90,9400
-0.41 %Makubaliano hayo yatatoa fursa kwa sekta ya uvuvi ya Uturuki kufikia bahari ya Somalia na una lengo la kutengeneza za ajira mpya kwa watu wa Somalia na kufanya taifa hilo kufikia biashara ya kimataifa.
Shirika la Uturuki la OYAK na Wizara ya Uvuvi na Uchumi unaotokana na Maji ya Somalia wametia saini makubaliano ya ushirikiano kuhusu shughuli za uvuvi katika maeneo ya bahari ya Somalia.
Makubaliano hayo yatatoa fursa kwa sekta ya uvuvi ya Uturuki kufikia bahari ya Somalia na una lengo la kutengeneza za ajira mpya kwa watu wa Somalia na kufanya taifa hilo kufikia biashara ya kimataifa.
Makubaliano hayo yalitiwa saini siku ya Jumatano kati ya Waziri wa Uvuvi wa Somalia Ahmed Hassan Aden na Meneja Mkuu wa OYAK Murat Yalçıntaş.
Miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo jijini Ankara ni Waziri wa Masuala ya Bandari wa Somalia Abdülkadir Muhammed Nur, Waziri wa Ulinzi wa Uturuki Yaşar Güler na Mkuu wa Majeshi ya Uturuki Selçuk Bayraktaroğlu. Wengine waliokuwepo ni Mwenyekiti wa Bodi ya OYAK Zekai Aksakallı.
Makubaliano hayo “yanajumuisha usimamizi endelevu wa shughuli za uvuvi nchini Somalia, kulinda raslimali za baharini, na kutoa leseni, ufuatiliaji, na kuratibu shughuli zote za uvuvi katika bahari ya Somalia na maeneo maalum ya kiuchumi,” Wizara ya Ulinzi ya Uturuki ilisema katika taarifa.
Katika makubaliano hayo, kampuni ya SOMTURK ilianzishwa kushughulikia masuala yote ya leseni yanayohusiana na uvuvi katika maeneo maalum ya uchumi nchini Somalia.
“Katika mfumo huu, leseni za uvuvi katika maeneo ya bahari ya Somalia zitatolewa na SOMTURK pekee; shughuli zitasajiliwa, zitafuatiliwa, na kuratibiwa," taarifa hiyo ilisema.
Makubaliano hayo yataimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili na yanalenga kuimarisha biashara ya samaki.
Comments
No comments Yet
Comment