Hatua ya dharura ya usalama wa mifugo yafuatia mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa miguu na midomo (FMD) nchini Afrika Kusini.

Zambia Yafunga Mpaka kwa Mifugo Kutoka Afrika Kusini
  • Serikali ya Zambia imesitisha mara moja uingizaji wa mifugo na bidhaa zote zinazohusiana na mifugo kutoka Afrika kusini, kufuatia kuenea kwa ugonjwa wa miguu na midomo (FMD) ambao umepelekea Pretoria kutangaza hali ya janga la kitaifa.

    Wizara ya Uvuvi na Mifugo ya Zambia ilitangaza kuwa vibali vyote vya awali vya kuingiza mifugo kutoka Afrika Kusini vimefutwa mara moja.

    Msemaji wa wizara hiyo, Benny Munyama, alisema hatua hiyo imechukuliwa kulinda sekta ya mifugo ya nchi dhidi ya maambukizi. Marufuku hiyo haihusishi tu mifugo hai, bali pia inajumuisha vyakula vya mifugo, ngozi, bidhaa za wanyama wenye kwato zilizogawanyika pamoja na maziwa na bidhaa zake, isipokuwa pale hatua kali za kudhibiti maambukizi zitakapotekelezwa.

    Aidha, usafirishaji wa mifugo hai kutoka Afrika Kusini kupitia Zambia kuelekea nchi nyingine pia umesimamishwa hadi hali itakapotengamaa.

  • Chanzo: Afrikanews

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#