Sport
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa aanza ziara ya siku mbili Algeria kujadili masuala ya uhamiaji na mapambano dhidi ya ugaidi.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa, Laurent Nuñez, ameanza ziara ya siku mbili nchini Algeria kwa lengo la kufufua ushirikiano wa kiusalama kati ya Paris na Algiers, wakati ambapo uhusiano wa kidiplomasia bado uko katika hali tete.
Nuñez amesema anawasili na “nia ya kujenga upya mazungumzo ya kiusalama,” hasa katika nyanja za uhamiaji, mapambano dhidi ya ugaidi na biashara haramu ya dawa za kulevya.
Moja ya masuala nyeti yanayotarajiwa kujadiliwa ni kurejeshwa kwa raia wa Algeria walioko Ufaransa bila vibali halali vya ukaazi na waliowekewa amri ya kuondoka nchini (OQTF). Vyanzo vya karibu na mazungumzo hayo vinasema bado hakuna raia aliyepokelewa rasmi na Algiers chini ya utaratibu huo.
Kuhusu kesi ya mwanahabari wa michezo wa Ufaransa, Christophe Gleizes, aliyekamatwa mwaka 2024 na kuhukumiwa kifungo kwa madai ya “kuunga mkono ugaidi”, Nuñez ameeleza kuwa suala hilo liko mikononi mwa mahakama za Algeria na halitakuwa ajenda kuu ya ziara yake, ambayo inalenga zaidi masuala ya usalama.
Chanzo: AA
Comments
No comments Yet
Comment