Dollar

0,0000

%

Euro

0,0000

%

Gram Gold

0,0000

%

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Wapiganaji wa RSF waliwapiga risasi wanaume waliokuwa wakitoroka mji wa al Fasher uliozingirwa kwa muda mrefu baada ya kuuteka, kulingana na mmoja wa walioshuhudia na kufanikiwakutoroka, taarifa iliyothibitishwa na wafanyakazi wa mashirika ya misaada

Wataalamu waonya kuhusu uwezekano wa vita vya kikabila Sudan

Mashirika ya misaada na wanaharakati wameonya kuhusu uwezekano wa mashambulizi ya kulipiza kisasi yaliyochochewa kikabila huku wapiganaji wa Rapid Support Forces (RSF) wakilizidi jeshi pamoja na vikosi washirika, wengi kutoka kabila la Zaghawa.

Wapiganaji wa RSF nchini Sudan waliwapiga risasi wanaume waliokuwa wakitoroka kutoka mji al Fasher uliozingirwa kwa muda mrefu baada ya kuuteka, kulingana na mmoja ya walioshuhudia na kufanikiwa kutoroka, taarifa iliyothibitishwa na wafanyakazi wa mashirika ya misaada, picha za satelaiti, na video za mitandao ya kijamii ambazo hazijathibitishwa.

Ushindi wa wapiganaji hao baada ya kuzingira mji kwa miezi 18 unaimarisha udhibiti wake wa Darfur, ambapo wamekuwa wakishutumiwa kwa mauaji ya kikabila, na kuchochea mgawanyiko nchini kutokana na kuunda serikali pinzani.

Wataalamu wanasema RSF inaweza kutumia kasi hiyo kujaribu kupanua eneo lake.

Vita vya miaka miwili na nusu kati ya RSF na jeshi vimesababisha kile Umoja wa Mataifa unaasema kuwa mgogoro mkubwa zaidi kwa watu duniani.

Njaa kali imekithiri, al-Fasher ilikuwa moja ya maeneo ambayo yalikumbwa na njaa. Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani katika mji huo yalilenga hospitali na mikusanyiko mingine ya watu.

Kiongozi wa wapiganaji wa RSF, Mohamed Hamdan Dagalo, anayejulikana kama Hemedti, alisema katika hotuba iliyotolewa Jumatano (Oktoba 29) kwamba watu waliokimbia mji wa Darfur wa al-Fasher wanatakiwa kurejea nyumbani.

Pia alitangaza kuunda kamati ya kuchunguza kile alichokitaja kuwa ni “ukiukwaji” uliofanyika mjini humo, uliotekelezwa na vikosi yake hivi karibuni.

“Kamati ya uchunguzi itaanza mara moja kuchunguza na kumuajibisha askari yeyote au ofisa yeyote aliyefanya uhalifu au kuvuka mipaka dhidi ya mtu yeyote, watakamatwa mara moja na matokeo (ya uchunguzi) kutangazwa mara moja na hadharani mbele ya kila mtu,” alisema.

Al-Fasher, ngome muhimu kubwa ya mwisho ya jeshi la Sudan katika eneo la magharibi la Darfur, ilitwaliwa na RSF siku ya Jumapili (Oktoba 26).

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#