Sport
Dollar
42,0751
0.17 %Euro
48,7444
0.06 %Gram Gold
5.447,8700
0.32 %Quarter Gold
9.212,2300
0 %Silver
66,2200
0.28 %Hospitali ya mwisho inayofanya kazi katika mji wa Al Fasher, Sudan, imeshambuliwa na mamia ya watu wanahofiwa kufariki baada ya wanamgambo kuudhibiti mji huo wiki hii, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) na afisa wa Sudan wamesema.
 
                    Shirika la habari la Reuters halikuweza kuthibitisha vifo hivyo mara moja, kwa kuwa mawasiliano ndani ya mji huo yamekatika na madaktari kutoka hospitali hiyo hawajapatikana kwa mawasiliano tangu wanamgambo wa RSF wachukue udhibiti kambi ya mwisho ya jeshi la Sudan mjini humo siku ya Jumapili.
Haikuwa wazi ni lini hasa shambulio hilo lilitokea, ambalo afisa wa Sudan pamoja na madaktari na wanaharakati wamelishutumu RSF kwa mashambulizi hayo.
Zaidi ya watu 36,000 wamekimbia Al Fasher tangu Jumapili, kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Wakimbizi (IOM), hata hivyo hakuna taarifa kamili kuhusi hatma ya zaidi ya watu 200,000 wanaodhaniwa kubaki mjini humo wakati wa mashambulizi ya RSF na mzingiro kwa miezi 18.
Gavana asema ‘mamia waliuawa’
Mashirika ya haki za binadamu yamekuwa yakihofia kuwa udhibiti wa Al Fasher na RSF kunaweza kusababisha mauaji ya halaiki ya kulipiza kisasi, na wale waliokimbia kutoka mji huo wameripoti mauaji ya dhulma kutekelezwa.
Mashirika ya haki na maafisa wa Marekani wamewatuhumu wapiganaji wa RSF na washirika wake kwa kufany mauaji ya kikabila huko Darfur.
Al Fasher ilikuwa kambi ya mwisho muhimu ya jeshi katika eneo kubwa la Magharibi Darfur katika vita vinavyoendelea kati ya jeshi na RSF, vita ambavyo vilianza tangu Aprili 2023.
Gavana wa Jimbo la Darfur, Minni Minawi, ambaye awali alikuwa kiongozi wa waasi wa Darfur lakini sasa aliyeungana na jeshi dhidi ya RSF, alisema Jumatano kwenye mtandao wa kijamii wa X kuwa watu 460 waliuawa katika shambulio dhidi ya Hospitali ya Saudi mjini Al Fasher.
Hata hivyo Minawi hakutoa ufafanuzi zaidi. Vikundi viwili vya madaktari wa Sudan, vikiwa na vyanzo kutoka Al Fasher, na kundi la wanaharakati wa Al Fasher, walisema wanadhani mamia ya watu waliokuwa kwenye vyumba vya muda vya wagonjwa karibu na hospitali pia waliuawa, pamoja na wale waliokuwa ndani ya hospitali. Hata hivyo shirika la habari la Reuters haikuweza kuthibitisha madai hayo.
Wafanyakazi wa afya watekwa
Shirika la WHO limesema kwenye taarifa Jumatano kuwa madaktari wanne, muuguzi mmoja, na mfamasia mmoja walitekwa kutoka Hospitali ya Saudi. Hata hivyo shirika hilo la kibinadamu halikuweza kuthibitisha idadi ya waliokufa, lakini limethibitisha tukio la utekaji.
Msemaji wa WHO aliliambia shirika la Reuters kuwa shambulio hilo limehakikishwa kupitia kauli za mashahidi wengi, ukarasa wa serikali, na picha na video.
Video iliyosambazwa na Minawi na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ilionekana kuonyesha shambulio dhidi ya hospitali, lakini Reuters ilibaini kuwa eneo lililopo siyo hospitali bali jengo la Chuo Kikuu cha Al Fasher lililotumika kama hifadhi ya wakazi.
Hata hivyo, picha za satelaiti za hospitali zilizochapishwa Oktoba 28 na Yale Humanitarian Research Lab zilionyesha makundi ya vitu vyeupe vilivyozungushwa na madoa mekundu ardhini, vinavyolingana na miili ya binadamu karibu na hospitali.
Makombora na ndege zisizo na rubani
Kwa mujibu wa wakazi wa Al Fasher, madaktari, na wahudumu wa kutoa misaada ya kibinadamu, RSF ilishambulia mara kwa mara hospitali ndani ya Al Fasher, kwa kutumia roketi, ndege zisizo na rubani, na kupitia wapiganaji wa ardhini.
Wakati wa mji huo ulipozingirwa na RSF, madaktari waliokuwa wamebaki Al Fasher walikuwa wakitibu utapiamlo, majeraha, na uzazi katika Hospitali ya Saudi huku vifaa vikiwa vichache, baada ya wagonjwa kukimbia hospitali zingine kutokana na mashambulio.
Comments
No comments Yet
 
                     
                 
                 
             
                                         
                                         
                                         
                                         
                                         
                                         
                                         
                                         
                                 
                             
                                 
                                 
                                 
                                 
                 
            
Comment