Mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani yamezidisha hali mbaya kwa watu nchini Sudan, kuwaua ambao walikuwa wameondoka katika makazi yao Kordofan Kaskazini na kuongeza idadi ya waliofariki kwenye vita vinavyoendelea.

Wapiganaji wa Sudan RSF wafanya mashambulizi ya droni, kuwaua watu kadhaa ikiwemo watoto

Mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani ya wapiganaji wa Sudan yalilenga gari lililokuwa limebeba familia zilizokuwa zimeondoka kwenye makazi yao katikati mwa nchi siku ya Jumamosi, na kuwaua watu wasiopungua 24, ikiwemo watoto wanane, shirika la madaktari limesema.

Shambulio hilo la Rapid Support Forces (RSF) limetokea karibuy na mji wa Rahad mkoa wa Kordofan Kaskazini, lilisema shirika la Mtandao wa Madktari wa Sudan, ambalo linafuatilia vita vinavyoendelea nchini humo.

Gari hilo lililokuwa likisafirisha watu waliokimbia makazi yao kutokana na vita huko eneo la Dubeiker Kordofan Kaskazini, shirika hilo la madktari limesema katika taarifa.

Miongoni mwa waliofariki walikuwa watoto wawili wachanga, kundi hilo limesema.

Kuongezeka kwa vifo vya watoto

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya watoto liliripoti siku ya Ijumaa kuwa watoto wasiopungua 20 waliuawa mwezi Januari nchini Sudan, wengi wao maeneo ya Kordofan na Darfur magharibi mwa Sudan.

Shirika hilo limeonya kuwa “mamilioni ya watoto nchini Sudan wanahitaji misaada, ulinzi na kurudishwa kwa huduma za msingi” wakati mapigano yakiendelea kuharibu maeneo mengi ya nchi.

UNICEF inasema njaa kali tayari imethibitishwa Al Fasher Kaskazini mwa Darfur na Kadugli huko Kordofan, huku maeneo mengine karibu 20 yakiwa hatarini.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#