Dollar

40,5757

0.05 %

Euro

46,9793

-0.1 %

Gram Gold

4.339,4800

0.39 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Uturuki imeutaka Umoja wa Mataifa kuchukua hatua madhubuti kuhusu suala la dola ya Palestina, ikionya kuwa vitendo vya Israeli vinafifisha matumaini ya kuwa na suluhu ya dola mbili.

Uturuki yailaumu Israel kwa kuzuia upatikanaji wa dola ya Palestina

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Nuh Yılmaz ameilalamikia Israel kwa kuwa vikwazo kwa kupatikana kwa dola ya Palestina, akitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuacha kutoa kauli tu, bali kuchukua hatua madhubuti ya kupata suluhu ya dola mbili.

“Ni wazi kuwa ukaliaji wa mabavu unaofanywa kwa sasa ni kikwazo kikubwa kwa dola ya Palestina,” alisema Yilmaz siku ya Jumatatu wakati wa kikao cha ngazi ya juu ca Umoja wa Mataifa kilichofanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York.

Pia aliipongeza uamuzi wa hivi karibuni wa Ufaransa wa kuitambua dola ya Palestina, akisema kuwa Ankara ina matumaini kuwa “wengine watafanya vivyo hivyo.”

Kulingana na Yılmaz, mrejesho alioupata kutoka wajumbe wa mkutano huo, ni dhihirisho tosha la hofu ya ulimwengu kuhusu mateso ya watu wa Palestina.

Uwezeshwaji wa dola huru ya Kipalestina

Aliongeza kuwa, hoja nyingi wakati wa kikao hicho, ziliunga mkono ujenzi wa mamlaka ya Kipalestina, akisisitizia haja ya kuwa na dola huru ya Kipalestina.

Usitishwaji wa kukaa kwa mabavu katika eneo hilo, ni moja ya hoja zilizotawala mazungumzo hayo.

Yılmaz alibainisha kuwa baadhi ya wajumbe walipendekeza kuwepo mfumo wa usimamizi wa sheria ya kimataifa na viwango vya kibinadamu.

Pia aliangazia wito wa kuwawekea vikwazo walowezi wa Israel waliopo Ukingo wa Magharibi na Yerusalemu Kusini, akisema kuwa Israel inaweza kuwekewa shuruti.

‘Sitisha uhamishaji wa Wapalestina’

Mbali na hali mbaya ya Gaza, Yılmaz alianisha uporaji wa ardhi, uvunjaji makazi katika eneo la Ukingo wa Magharibi.

“Matendo ya Israel yanapaswa kuzuiwa bila kuchelewa. Hatuwezi kuwa na dola ya Palestina bila taifa la Palestina,” alisema.

Wakati wote wa kikao, wajumbe walisisitizia umuhimu wa utekelezwaji wa dola mbili.

“Inatupa ujumbe kuwa: Ni lazima jumuiya ichukue hatua kutengeneza mazingira ya dola mbili,” alisema Yılmaz.

 

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#