Sport
Dollar
40,5764
0.05 %Euro
46,9668
-0.13 %Gram Gold
4.341,4900
0.43 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Rais wa Uturuki agusia suala la usuluhishi Istanbul ikijiandaa na kuandaa awamu ya tatu ya mazungumzo ya amani kati ya Urusi na Ukraine.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameonesha matumaini yake kuwa Uturuki, kwa mara nyingine tena, itakuwa mwenyeji wa mazungumzo ya amani kati ya Urusi na Ukraine, akibainisha utayari wa Ankara katika kusasisha lengo la kumaliza vita.
“Kama vile tu meza ya majadiliano [kati ya Urusi na Ukraine] ilivyoanzishwa Istanbul, mazungumzo hayo ya amani yataendelea nchini Uturuki ndani ya siku chache zijazo, na umwagaji damu huu utaisha”, alisema Erdogan siku ya Jumatatu, mara baada ya kikao cha mawaziri jijini Ankara.
Kauli yake inakuja siku chache baada ya Istanbul kuwa mwenyeji wa mazungumzo ya amani kati ya Ukraine na Urusi ya Julai 23, baada ya hatua za awali zilizofanyika mwezi Mei na Juni.
Vikao hivyo vya ndani, vilihusisha maofisa wa kidiplomasia, huku Uturuki ikiripotiwa kufanikisha vikao kati ya washauri waandamizi na maofisa usalama kutoka pande zote mbili.
Juhudi za usuluhishi za Uturuki
Hapo awali, Ankara imewahi kuwa mwenyeji wa mazungumzo ya amani ya Machi 2022, wakati ambapo wajumbe kutoka Urusi na Ukraine kukutana jijini Istanbul kwa mazungumzo ya ana kwa ana, wiki chache baada ya kuanza kwa vita.
Licha ya majadiliano hayo kusuasua, bado yalitengeneza njia ya maazimio mbalimbali ikiwemo uliokuwa mkataba wa nafaka, ambao ulifikiwa kati ya Umoja wa Mataifa na Uturuki.
Uturuki imejiweka katika nafasi ya usuluhishi, ikiendeleza mahusiano yake na Kiev na Moscow.
Mara kwa mara, Erdogan amekuwa akijitolea kusuluhisha, akigusia haja ya kuwa na diplomasia badala ya kuchochea vita.
Ingawa, dondoo za vikao vilivyopita bado hazijajulikana, maofisa wa Uturuki wameyaita mazungumzo hayo kuwa ni ya ‘kiufanisi’, yenye malengo ya kutengeneza mazingira ya amani.
Juhudi za Rais Erdogan za kukumbatia diplomasia, zinakuja wakati ambapo kuna sintofahamu ya kijeshi nchini Ukraine.
Comments
No comments Yet
Comment