Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa yote mawili walikutana mjini Kiev kujadili uhusiano wa pande zote mbili na ushirikiano wa kiuchumi.

Ukraine yatoa onyo kwa raia wa Ghana kutojiunga na majeshi ya Urusi

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Andrii Sybiha, amewaonya raia wa Ghana dhidi ya kujiunga na majeshi ya Urusi katika mzozo wa Ukraine, akisema kuwa Urusi inawasajili raia wa kutoka nchi za Afrika ili wapigane upande wake.

Waziri huyo alimpokea mwenzake kutoka Ghana, Samuel Okudzeto Ablakwa, mjini Kiev siku ya Jumatano, ambapo walijadiliana juu ya kuimarisha mazungumzo ya kisiasa na ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.

Sybiha alisema nchi ya Ghana ni mshirika muhimu katika Afrika Magharibi na kusema Ukraine iko tayari kuanzisha kituo cha nafaka ya chakula nchini Ghana ili kuimarisha utulivu wa chakula duniani.

Aliipongeza Ghana kwa uungaji mkono thabiti kwa uhuru na mamlaka ya Ukraine, hasa kura yake ya kuunga mkono azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhsu Uungaji Mkono kwa Amani Endelevu nchini Ukraine.

“Tunapanua ushirikiano wetu katika usalama wa chakula, usafirishaji, sekta za ulinzi, elimu, na sekta nyinginezo. Tunatazamia uongozi wa Ghana katika Umoja wa Afrika mwaka ujao na tumezungumzia vipaumbele vyake,” alisema Sybiha.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#