Sport
Hatua hii ni sehemu ya kujumuisha Somalia katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Somalia inatarajiwa kuanza kutoa hati za kusafiria za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa raia wake, na kuungana na nchi wanachama wengine wanaotumia pasipoti hizo.
Balozai wa Somalia nchini Tanzania na Mwakilishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Ilyas Ali Hassan, amemkabidhi Waziri wa Mambo ya Ndani wa Somalia Jenerali Abdullahi Sheikh Ismail “Fartaag” na Mkurugenzi Mkuu wa Uhamiaji wa Somalia, Mustafa Sheikh Ahmed Dhuhulow hati yenye nembo ya Afrika Mashariki, nchini Tanzania siku ya Jumanne.
Hatua hii ni muhimu kidiplomasia kwa Somalia na inatarajiwa kuimarisha ushirikiano katika kanda na kurahisisha raia wa Somalia kufanya ziara bila vikwazo katika maeneo ya Afrika Mashariki.
Somalia imeidhinishwa kuchapisha hati za kusafiria za Afrika Mashariki Disemba 2025, kabla wiki hii kutolewa muundo wa pasipoti ulioidhinishwa.
Hati za kusafiria ya EAC ilianzishwa katika Mkutano wa 17 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki tarehe 2 Machi, 2016, ambapo viongozi pia walianzisha pasipoti za kielektroniki katika madaraja matatu - Diplomasia, watumishi wa umma na la kawaida.

Pasipoti a elektroniki, ambazo zinatambuliwa kimataifa, zilianzishwa kuchukua nafasi ya zile za mataifa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Wanachama wengine wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Kuanzishwa kwa hati hizo za kusafiria za Afrika Mashariki hatua kwa hatua kwa nchi zote wanachama kumeweka msisitizo wa kuainisha pasipoti katika kanda hiyo.
Somalia ilijiunga rasmi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kama nchi wanachama wa nane baada ya kuwasilisha nyaraka za Kuidhibishwa kw Makubaliano kwa Katibu Mkuu kwenye hafla iliyofanyika Makao Makuu ya EAC mjini Arusha, Tanzania, Machi 2024.
Hatua hii inafuatia kuidhinishwa kwa uanachama wa Somalia na viongozi wa kanda katika Mkutano wa 23 wa Wakuu wa Nchi wa EAC mjini Arusha.
Wanachama wengine ni Burundi, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Uganda.
Somalia tayari imeshateua wabunge tisa kwa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), ambao watawawakilisha katika makao makuu mjini Arusha, Tanzania.
Comments
No comments Yet
Comment