Sport
Dollar
40,1901
0.22 %Euro
47,1146
0.08 %Gram Gold
4.336,9600
1.24 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Mpaka huo ulifungwa mwishoni mwa mwezi Januari baada ya waasi wa M23 kuchukuwa udhibiti wa Goma, mji mkuu wa mkoa wa DRC wa Kivu ya Kaskazini.
Uganda imefungua tena mpaka wake na mashariki ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi wa M23, mamlaka zimesema siku ya Ijumaa.
Chris Magezi, msaidizi wa masuala ya kijeshi wa Mkuu wa Majeshi ya Uganda, alisema mpaka ulifunguliwa siku ya Alhamisi kufuatia agizo la Rais Yoweri Museveni.
“Mpaka kati ya Uganda na DRC katika eneo linalodhibitiwa na M23 sehemu ya Bunagana na Ishasha umefunguliwa. Hili linafuatiwa na agizo la Rais kupitia Mkuu wa Majeshi kufungua mpaka huo,” Magezi alisema katika taarifa kupitia mtandao wa X.
“Ilikuwa ni uhalifu na jambo lisilosaidia kuzuia biashara kati ya jamii mbili jirani ambazo zinategemeana. Wale waliofanya hivyo wanachunguzwa,” alisema.
Soko muhimu
Mpaka huo ulifungwa mwishoni mwa mwezi Januari baada ya waasi wa M23 kudhibiti Goma, mji mkuu wa Mkoa wa DRC wa Kivu Kaskazini.
Waasi wa M23 walizidisha mashambulizi yao mashariki mwa Congo Novemba 2021.
Sasa hivi waasi wanadhibiti maeneo muhimu mashariki mwa Congo, ikiwemo makao makuu ya mkoa Goma na Bukavu ambayo ilichukuwa udhibiti mapema mwaka huu. Waasi hao walichukua udhibiti wa mpaka wa Bunagana Juni 2022.
Desire Kanyamarere, afisa mmoja wa Congo, ameambia waandishi wa habari Alhamisi kuwa kufungwa kwa mpaka huo kumefanya wakazi wa pande zote mbili kukosa ajira.
Mkoa wa Kivu Kaskazini ulioko kusini mwa DRC ni soko muhimu kwa bidhaa za Uganda.
Comments
No comments Yet
Comment