Dollar

40,1901

0.22 %

Euro

47,1146

0.08 %

Gram Gold

4.336,9600

1.24 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Trump amekuwa akitaka wahamiaji waondolewe kwa haraka, ikiwemo kuwapeleka katika mataifa ya tatu.

Nigeria yakataa 'shinikizo' la Marekani kukubali wahamiaji wa Venezuela

Waziri wa mambo ya nje wa Nigeria anasema Marekani inashinikiza mataifa ya Afrika kuwapokea wahamiaji kutoka Venezuela, wengine wanatoka gerezani, lakini nchi yenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika haiwezi kuwapokea kutokana na matatizo yao wenyewe.

Wiki hii serikali ya Rais Donald Trump imewataka marais watano wa Afrika waliokuwa katika ziara Ikulu ya Marekani ya White House kuchukua wahamiaji kutoka mataifa mengine ambao wameondolewa Marekani, maafisa mawili wanaofahamu kuhusu mazungumzo hayo waliliambia shirika la habari la Reuters.

Yusuf Tuggar, waziri wa mambo ya nje wa Nigeria, ameviambia vyombo vya habari vya nchini kwake siku ya Alhamisi kuwa Nigeria haitokubali hilo.

"Inabidi utambuwe kuwa Marekani inaweka shinikizo kwa mataifa kadhaa ya Afrika kuwakubali wahamiaji wa Venezuela waliotimuliwa Marekani, wengine wanatoka gerezani kabisa," alisema akiwa Brazil, ambako anahudhuria kongamano la BRICS.

‘Matatizo ya kwetu wenyewe’

"Itakuwa vigumu kwa nchi kama Nigeria kukubali wafungwa kuingia nchini mwetu. Tuna matatizo ya kwetu wenyewe," akieleza kuhusu idadi ya watu wake milioni 230.

Tangu kurejea ofisini mwezi Januari, Trump amekuwa akiharakisha mchakato wa kuwaondoa wahamiaji, ikiwemo kuwapeleka katika mataifa ya tatu wakati kuna matatizo au kuchelewa katika kuwarudisha kwao.

Wiki hii, alikuwa mwenyeji wa marais wa Liberia, Senegal, Guinea-Bissau, Mauritania na Gabon katika Ikulu ya White House.

Kulingana na maafisa wa Marekani na Liberia, aliwasilisha mpango kwa mataifa ya Afrika kuwapokea wahamiaji kutoka nchi zingine wanapoondolewa Marekani.

Wiki iliopita, inasemekana wahamiaji wanane, waliokuwa wanahusishwa na uhalifu, waliondolewa Marekani na kupelekwa Sudan Kusini baada ya kesi zao mahakamani.

Kati ya wanane hao, ni mmoja tu ambaye anatoka Sudan Kusini. Wengine wawili kutoka Myanmar, wawili kutoka Cuba, na wengine mmoja mmoja kutoka Vietnam, Laos na Mexico.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#