Dollar

40,1733

0.22 %

Euro

47,0289

-0.04 %

Gram Gold

4.334,9100

1.19 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Tume hiyo inajiandaa na kuiongoza nchi hiyo kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka 2027.

Kenya: Mwenyekiti na Makamishna wa tume ya IEBC waapishwa rasmi

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya (IEBC), imeanza kazi rasmi kufuatia kuapishwa kwa wa mwenyekiti na makamishna wa tume hiyo..

“Tunayo furaha kutangaza kwamba, kufuatia kutangazwa rasmi kwa gazeti la serikali na kuapishwa kwa Mwenyekiti na Makamishna wapya…sasa, IEBC imeundwa rasmi na ipo tayari kwa kazi,” alisema Erastus Edung Ethekon, mwenyekiti wa IEBC.

Makamishna walioapishwa ni Anne Njeri Nderitu, Moses Alutalala Mukhwana, Mary Karen Sorobit, Hassan Noor Hassan, Profesa Francis Odhiambo Aduol na Fahima Araphat Abdallah.

“ Leo ni mwanzo wa huduma yetu kwa Kenya, lazima tuongozwe na Katiba yetu na matarajio ya Wakenya,” alisisitiza Ethekon, mara baada ya kula kiapo mbele ya Jaji Mkuu, Martha Koome.

Tume hiyo inatarajiwa kuongoza nchi hiyo kwa uchaguzi mkuu wa 2027.

“ Uchaguzi huru, wa haki, na wa kuaminika ndio msingi wa demokrasia yetu. Uaminifu wangu ni kwa watu wa Kenya, na ninawahakikishia, sauti zao zitasikika na zitahesabiwa. Ni lazima tujenge taifa thabiti, uchaguzi mmoja baada ya mwingine.”

Kwa upande wake, Jaji Koome aliwataka wajumbe hao wa IEBC kutimiza kikamilifu kwa matakwa ya kisheria wakati wa kufanya majumu yao.

“Sherehe hii ya kuapishwa haihusu tu kutimiza matakwa ya kisheria bali inahusu uhamishaji wa uaminifu uliohamishwa kwako na Wakenya…kilio kikubwa katika pande zote za nchi ni uadilifu, uwajibikaji na haki. Ni wajibu wako kuhakikisha demokrasia yetu inalindwa na kuheshimiwa,”alisema Jaji Koome baada ya kuwaapisha wajumbe hao.

"Kenya si mali ya wanasiasa. Si mali ya mahakama. Sio ya IEBC, polisi au taasisi nyingine yoyote. Kenya ni yetu sote, na hakuna aliye na haki ya kukanyaga wengine," alisema.

Jaji Koome, pia amewataka wajumbe hao kufanya kazi kwa weledi, ujasiri, kujitoa na kuepuka kutoa upendeleo wa aina yoyote wakati wa kutimiza majukumu yao.

Alionya dhidi ya kuibuka kwa migogoro ya ndani ya IEBC, akiwataka wajumbe hao kufanya kazi kwa vitendo na si maneno peke yake.

"Bila shaka kuna upungufu mkubwa wa uaminifu wa umma, haswa kati ya serikali na raia, ambayo unahitaji ushiriki wa dhati ili tuujenge upya," alieleza Jaji Koome.

Kulingana na Jaji Koome, ni vyema kwa IEBC kufanya maandalizi ya haraka kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2027, ukizingatia kuwa Kenya imekuwa bila ya tume kamili kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili.

"Pengo hili la kitaasisi limechelewesha michakato kadhaa muhimu ambayo ni muhimu kwa afya ya kidemokrasia ya Kenya," alibainisha.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#