Sport
Dollar
43,4748
-0.04 %Euro
51,2380
-0.7 %Gram Gold
6.506,4000
-4.16 %Quarter Gold
11.661,9400
-2.17 %Silver
110,9200
-4.78 %Tyla ashinda Grammy ya Best African Music Performance kwa mara ya pili.
Mwanamuziki chipukizi kutoka Afrika Kusini, Tyla, ameweka alama ya kipekee katika historia ya muziki wa dunia kwa kushinda tuzo ya Grammy ya Best African Music Performance kwa mara ya pili. Ushindi huu wa mwaka 2026 unatokana na wimbo wake “Push 2 Start”, ambao umevutia mashabiki kwa kuchanganya mitindo ya pop, R&B na Amapiano.
Kwa ushindi huu, Tyla anakuwa msanii wa kwanza kutwaa tuzo hiyo mara mbili tangu kuanzishwa kwake mwaka 2024. Akiwa na umri wa miaka 24, aliwashinda mastaa wakubwa wa Afrobeats kutoka Nigeria kama Burna Boy, Davido, Wizkid, Ayra Starr, Omah Lay, pamoja na Eddy Kenzo wa Uganda.
Tyla alishinda tuzo hiyo kwa mara ya kwanza mwaka 2024 kupitia wimbo wake maarufu “Water”, na wakati huo alikuwa mshindi mdogo zaidi wa kipengele hicho. Akizungumza baada ya ushindi wa sasa, alisisitiza shukrani kwa mashabiki wake na vijana wa Kiafrika, akisema: “Kamwe msione aibu kwa asili yenu, sisi ni moto.”
Ushindi huu unaonekana kama ishara ya kupaa kwa muziki wa Afrika katika jukwaa la kimataifa. Katika hafla hiyo hiyo ya Grammy, gwiji wa Afrobeat kutoka Nigeria, Fela Kuti, alitunukiwa tuzo ya heshima ya Lifetime Achievement Award, na kuwa msanii wa kwanza wa Kiafrika kupata heshima hiyo.
Comments
No comments Yet
Comment