Sport
Dollar
40,2274
0.14 %Euro
46,9980
-0.17 %Gram Gold
4.323,1900
-0.27 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Mwakilishi wa Wanawake wa Wajir Fatuma Jehow, aliyesema waziwazi kwamba viongozi kutoka eneo la Kaskazini Mashariki mwa Kenya 'wangeiba kura kwa niaba ya' Rais Ruto katika Uchaguzi Mkuu wa 2027.
Tume ya Uchaguzi nchini Kenya imewaonya wale wanaotoa matamshi potofu kuhusu uchaguzi.
“Tume ina wasiwasi kuhusu taarifa kuhusu tuhuma potofu za uchaguzi nchini. Matamshi kama haya hayatokubalika,” IEBC imesema katika taarifa.
IEBC imekashifu vikali matamshi ya hivi majuzi ya Mwakilishi wa Wanawake wa Wajir Fatuma Jehow, ambaye alipendekeza wazi wazi kwamba viongozi kutoka eneo la Kaskazini Mashariki 'wangeiba kura kwa niaba ya' Rais Ruto katika Uchaguzi Mkuu wa 2027.
Akiongea katika mkutano wa umma mjini Wajir 12 Juali 2025, Jehow alisema.
“Sisi wabunge wa Kaskazini Mashariki hatuna maneno ya Rais, tunasema ‘tutam’( mihula miwili kwake), hata kama hatutakua na kura tutamwibia… hio si siri.”
Tume ya IEBC imetaja matamshi kama haya kuwa yasiyokubalika.
“Tume inawataka wadau wote hasa wale walio katika ulingo wa kisiasa kujiepusha na vitendo vikiwemo hotuba zinazoweza kuondoa uaminifu katika michakato yetu ya uchaguzi, na badala yake kufanya kazi nasi ili kuimarisha imani hiyo na kujiamini,” IEBC imesema.
“Matamshi haya hayajali jamii ya kidemokrasia kama yetu, na IEBC inawataka Wakenya wote kupuuza au kujitenga nayo.”
“Ikumbukwe kuwa IEBC haijatangaza uchaguzi wowote. Zaidi, hakuna gazeti la serikali au tamko ambalo limetolewa kuthibitisha matamshi kama hayo ya kisiasa na propaganda. Nchi haiko kwenye kipindi cha kampeni kwa sasa,” IEBC imeonya.
Mweneyekiti wa IEBC na makamishna wake wameapishwa hivi majuzi 11 Julai 2025.
“IEBC sasa imeundwa kikamilifu na itashirikiana na wadau wakiwemo vyama vya siasa na viongozi kujadili njia za kurejesha imani na kujiamini katika michakato na matokeo yetu ya uchaguzi.”
Kulingana na katiba ya Kenya Uchaguzi Mkuu unapashwa kufanyika mwaka 2027. Rais wa sasa Willim Ruto anayekabiliwa na changamoto ya baadhi ya wananchi kupinga sera zake, anatarajiwa kuwania muhula wa pili.
Comments
No comments Yet
Comment