Dollar

40,2275

0.13 %

Euro

46,9162

-0.35 %

Gram Gold

4.329,3000

-0.13 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Mawaziri kutoka kote barani Afrika pamoja na wanaharakati wa mazingira na watunga sera wakutana kwa kikao cha ishirini cha mawaziri kujadili mazingira kuambatana na miaka arobaini tangu kuundwa kwake.

Kikao cha mawaziri wa mazingira barani Afrika AMNCEN, chang'oa nanga jijini Nairobi

Mawaziri wa mazingira kutoka kote barani Afrika wameanza kikao chao jijini Nairobi Kenya kikiwa kikao cha ishirini tangu kuundwa kwa bodi hiyo.

AMCEN-20 kama inavyofahamika zaidi, inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 40 ya AMCEN, ikitoa jukwaa muhimu kwa mawaziri na washikadau wa Afrika kutathmini maendeleo, kushiriki maarifa, na kuweka mikakati kuhusu vipaumbele vya mazingira vya bara.

Kikao hicho kinalenga kuimarisha ushirikiano wa kikanda huku Afrika ikiendelea kukabiliana na changamoto za kimazingira na kutafuta maendeleo endelevu.

Kikao hicho kinachoandaliwa kwa udhamini wa serikali ya Libya, kinatazamiwa kuangazia mafanikio muhimu katika miongo minne iliyopita huku ukizingatia masuluhisho ya kiubunifu ili kupata mustakabali wa mazingira wa Afrika.

Sauti moja ya Afrika katika jukwaa la kimataifa

AMCEN ilianzishwa Desemba 1985, kufuatia mkutano wa mawaziri wa mazingira wa Afrika huko Cairo, Misri. Kama chombo kinachoongoza katika ngazi ya mawaziri katika masuala ya mazingira, AMCEN inatoa mwongozo wa kisiasa na uongozi wa kikanda ili kukuza usimamizi mzuri wa mazingira na maendeleo endelevu kote barani Afrika.

Kupitia sera, maazimio, na mipango ya utekelezaji, AMCEN inawezesha nchi za Afrika kushirikiana katika vipaumbele muhimu vya mazingira—kama vile hatua za hali ya hewa, uhifadhi wa viumbe hai, urejeshaji wa ardhi, kemikali na udhibiti wa uchafuzi wa mazingira, na ufadhili endelevu.

Mamlaka yake ya kuitisha huwaleta pamoja mawaziri, wataalam, mashirika ya kiraia, na washirika wa maendeleo ili kuoanisha juhudi za kikanda na kukuza sauti ya Afrika katika jukwaa la kimataifa.

Mkutano huo utaendelea hadi Julai 18, ambapo washiriki watatoa azimio jipya kwa mustakbali wa uhifadhi wa mazingira barani Afrika.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#