Dollar

40,2989

0.1 %

Euro

46,9561

-0.45 %

Gram Gold

4.323,8000

0.11 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Serikali ya Nigeria imetangaza siku ya Jumanne, Julai 15 sikukuu ya kitaifa kumuenzi aliyekuwa Rais wa nchi hiyo ambaye amefariki dunia Muhammadu Buhari.

Nigeria yatangaza siku ya Jumanne, Jula 15 sikukuu ya kitaifa kumuenzi Buhari

Serikali ya Nigeria imetangaza Jumanne, Julai 15 kuwa sikukuu ya kitaifa kwa lengo la kumuenzi aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Muhammadu Buhari, ambaye amefariki dunia.

Waziri wa Mambo wa Ndani wa Nigeria Olubunmi Tunji-Ojo, ambaye ametangaza sikukuu hiyo, alisema Jumatatu kuwa siku hiyo itakuwa kutoa heshima kwa Buhari kutokana na utumishi wake kwa taifa.

"Rais Muhammadu Buhari alitumikia Nigeria kwa dhati, maadili, na kujitolea kwa umoja na maendeleo ya taifa hili tukufu," Tunji-Ojo alisema katika taarifa.

"Sikukuu hii inatoa fursa kwa raia wote wa Nigeria kutafakari kuhusu maisha yake, uongozi wake na maadili aliyoyasimamia," aliongeza.

Siku saba za maombolezo

Buhari alifariki akiwa na umri 82 wakati akitibiwa katika hospitali moja jijini London nchini Uingereza siku ya Jumapili.

Serikali ya Nigeria inasema kiongozi huyo wa zamani wa nchi alifariki kutokana na "kuugua kwa muda mrefu", bila kueleza Buhari alikuwa akiumwa nini.

Siku ya Jumapili, Rais Bola Tinubu alitangaza siku saba za maombolezo ya kitaifa, na kumuagiza Makamu wa Rais Kashim Shettima kusafiri hadi Uingereza ili kusindikiza maiti ya Buhari nyumbani.

Shettima ameshafika London tayari.

Bahati mara ya nne

Katika matangazo yake, Rais Tinubu pia aliagiza bendera zote kupepea nusu mlingoti wakati taifa hilo la Afrika Magharibi likimuomboleza kiongozi wake wa zamani.

Buhari alichaguliwa kuwa rais kwa mihula miwili mfululizo, baada ya kushinda uchaguzi wa 2015 na 2019.

Kabla ya hapo, aliwahi kugombea mara tatu bila mafanikio, 2003, 2007 na 2011.

Hata hivyo Buhari, amekuwa kiongozi wa nchi wa kijeshi kuanzia Disemba 1983 hadi Agosti 1985 baada ya wanajeshi kupindua serikali ya aliyekuwa Rais Shehu Shagari kutokana na "changamoto za kiuchumi na ufisadi serikalini."


Kupinduliwa kwa Buhari

Agosti 1985, Meja Jenerali Ibrahim Babangida aliongoza mapinduzi dhidi ya serikali ya Buhari kutokana na ‘‘kushindwa kutatua matatizo ya kiuchumi ya Nigeria.’’

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#