Sport
Dollar
40,2338
0.13 %Euro
47,0554
0.33 %Gram Gold
4.328,6600
0.23 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Muda rasmi wa kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Malawi Septemba 16 umezinduliwa siku ya Jumatatu, huku kukiwa na hofu ya kisiasa katika nchi hiyo.
Kampeni zimezinduliwa rasmi Jumatatu kwa ajili ya uchaguzi mkuu nchini Malawi wa Septemba 16, huku kukiwa na wasiwasi kuhusu machafuko ya kisiasa.
Kulingana na Tume ya Uchaguzi ya Malawi, watu milioni 7.2 wamejisajili kwa ajili ya uchaguzI wa saba wa taifa hilo tangu lilipoanza siasa ya vyama vingi 1993 baada ya utawala wa miaka 30 wa chama kimoja.
Akizungumza wakati wa uzinduzi katika mji mkuu Lilongwe, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Malawi Annabel Mtalimanja amehakikisha kuwa tume “iko tayari kufanya uchaguzi wa huru, na wa haki kwa Wamalawi.”
“Tuko tayari kusimamia mchakato wa uchaguzi ambao uko wazi na wa kuwajibika kwa wadau wote. Tunafanya kazi kulingana na sheria kuhakikisha kuwa hakuna machafuko tukielekea kwenye uchaguzi na kwamba baada ya uchaguzi kutakuwa na amani,” alisema Mtalimanja.
Tume ya uchaguzi inakabiliwa na madai ya upendeleo
Katika siku za hivi karibuni, vyama kadhaa vya kisiasa na vya kijamii vimeishtumu tume ya uchaguzi kwa upendeleo kwa chama tawala cha nchi hiyo Malawi Congress Party, madai ambayo tume hiyo imekuwa ikikanusha.
Kwa karibu wiki mbili, makundi ya mashirika ya kijamii yameandamana barabarani yakitaka Mtalimanja na Afisa Mkuu Mtendaji wa tume hiyo Andrew Mpesi kujiuzulu “kwa kufanya kazi dhidi ya upinzani.”
Rais Lazarus Chakwera, mmoja wa wagombea 17 wa urais, alionya wakati wa ibada ya Jumapili kuwa machafuko ya kisiasa huenda yakadumaza mafanikio ya demokrasia yaliyopatikana miaka kadhaa iliyopita.
“Tuweni na amani kati ya sasa na Septemba 16. Kwa njia yoyote sote tuepukane na mapigano. Amani imekuwa fahari ya nchi hii tangu tulipopata uhuru. Kipindi cha kampeni ni kifupi sana kwa hiyo tusifanye machafuko,” Chakwera alisema.
Polisi yawahakikishia raia wa Malawi kuhusu usalama
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi wa Malawi Noel Kayira ameuhakikishia umma kuwa polisi wako tayari kuweka usalama kwa wote watakaoshiriki kwenye uchaguzi.
“Kama taasisi ya usalama, tuko tayari na hatutobagua upande wowote wa kisiasa kuhakikisha kuwa tunafanya kazi kulingana na sheria kuhakikisha usalama kwa kila mtu anayeshiriki katika uchaguzi. Hatutoruhusu matukio yoyote ya uvunjifu wa sheria kutatiza mchakato wa uchaguzi,” Kayira alisema wakati wa uzinduzi.
Katika wiki za hivi karibuni, nchi hiyo imekuwa na matukio ya kuongezeka kwa machafuko yaliyochochewa kisiasa kati ya vyama pinzani, kusababisha majeraha na uharibifu wa mali ya umma na binafsi.
Comments
No comments Yet
Comment