Sport
Dollar
40,1761
0.23 %Euro
47,0500
0.03 %Gram Gold
4.335,7600
1.21 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Serikali ya Trump siku ya Jumatano iliwaomba marais watano wa Afrika kuwapokea wahamiaji kutoka nchi zingine wanapofukuzwa kutoka Marekani, Reuters imeripoti.
Wiki hii serikali ya Trump imewataka marais watano wa Afrika kuwapokea wahamiaji kutoka nchi zingine wanapofukuzwa Marekani, maafisa wawili wanaofahamu kuhusu mazungumzo hayo wameiambia Reuters siku ya Alhamisi.
Mpango huo uliwasilishwa kwa marais wa Liberia, Senegal, Guinea-Bissau, Mauritania na Gabon wakati wa ziara yao katika Ikulu ya Marekani ya White House siku ya Jumatano, kulingana na maafisa wa Marekani na Liberia ambao wote wameomba wasitambulishwe.
Wasemaji wa Ikulu ya Marekani na mataifa hayo matano hawakujibu walipotakiwa kueleza kuhusu hayo. Haikufahamika kama nchi hizo zilikubaliana na mpango huo.
Tangu kurejea ofisini mwezi Januari, Rais wa Marekani Donald Trump amekuwa akitaka kuwaondoa wahamiaji Marekani, ikiwemo kuwapeleka katika nchi ya tatu wakati kunapokuwa na tatizo au kuchelewa kuwapeleka makwao.
Kuwapeleka watu katika mataifa mengine ilikuwa sehemu ya agenda
Siku ya Jumamosi, wahamiaji wanane – kutoka Cuba, Laos, Mexico, Myanmar, Sudan na Vietnam, kulingana na wanasheria wao – waliwasili katika mji mkuu wa Sudan Kusini baada ya kushindwa katika kesi yao ya kusitishwa kuondolewa Marekani.
Mkutano wa Jumatano katika Ikulu ya White House uliandaliwa pia kwa sehemu kujadili kuhusu mpango wa kuwasafirisha wahamiaji, afisa huyo wa Marekani alisema. Serikali ya Liberia ilikuwa "inajiandaa kuwapokea" wahamiaji katika mji mkuu Monrovia, afisa wa Marekani aliongeza.
Afisa wa Liberia alithibitisha kuwa mpango wa kuwapeleka wahamiaji ulikuwa sehemu iliyoangaziwa kwenye mkutano wa Jumatano, lakini hakusema kama Rais wa Liberia Joseph Boakai alikubaliana na hilo.
Mfumo wa kutoka katika misaada hadi biashara
Chini ya mpango huo, serikali hazitowapeleka "wahamiaji katika mataifa yao au mataifa waliyokuwepo hadi pale maamuzi ya mwisho yatakapofanywa" kuhusu maombi yao ya hifadhi Marekani, kulingana na ripoti hiyo.
Reuters imeona nakala ya waraka wa Wizara ya Mambo ya Nje na haikuweza kuthibitisha kuhusu yaliyokuwemo ndani.
Katika taarifa kwa umma siku ya Jumatano, Trump aliwaambia viongozi hao watano kuna anabadilisha mtazamo wa Afrika kutoka kwenye misaada hadi katika suala la biashara, na kwamba Marekani ni mshirika mzuri zaidi kuliko China.
"Natumai tunaweza kupunguza idadi ya watu wanaoendelea kuishi baada ya muda wao wa viza kumalizika, na pia kuimarisha mipango ya usalama kwa mataifa watakayopelekwa," Trump aliongeza.
Alikuwa ameongozana na Massad Boulos, mshauri mwandamizi wa masuala ya Afrika, na mshauri wake Stephen Miller, ambaye ana msimamo mkali kuhusu suala la uhamiaji.
Comments
No comments Yet
Comment