Dollar

42,2154

0.26 %

Euro

48,9589

0.45 %

Gram Gold

5.419,6600

0.57 %

Quarter Gold

9.213,2100

0.59 %

Silver

65,5900

0.86 %

Miongoni walioshikwa ni mfanyabiashara, Jenifer Bilikwiza Jovin almaarufu Niffer amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam leo Ijumaa.

Tanzania yawashtaki watu 98 kwa uhaini

Waendesha mashtaka nchini Tanzania wamewashtaki watu 98 kwa kosa la uhaini siku ya Ijumaa, wakidaiwa kuhusika katika maandamano ya vurugu yaliyotokea wakati wa uchaguzi mkuu wa wiki iliyopita, kwa mujibu wa nyaraka za mahakama zilizoonekana na shirika la habari la Reuters.

Kwa mujibu wa nyaraka za Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Dar es Salaam, washtakiwa hao “walikusudia kuzuia uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa lengo la kutishia mamlaka ya Utendaji ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania” na waliharibu mali za serikali.

Mashtaka hayo ndiyo ya kwanza kufunguliwa dhidi ya watu wanaodaiwa kushiriki katika maandamano hayo.

Kiongozi mmoja wa dini alisema hatua hiyo ya serikali itazidisha mgawanyiko uliojitokeza wakati wa uchaguzi huo. Viongozi wa dini na wadau wengine wametoa wito kwa serikali kujaribu kuleta maridhiano na wapinzani wa kisiasa pamoja na waandamanaji.

Haya yanajiri baada ya Umoja wa Afrika (AU) kutoa ripoti kali kuhusu uchaguzi mkuu wa Tanzania wa mwaka 2025, ukisema kuwa mchakato huo umeshindwa kuheshimu misingi ya kidemokrasia, uwazi na haki.

Katika ripoti yake ya awali, Tume ya Uangalizi wa Uchaguzi ya AU ilibainisha kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa wa taratibu za uchaguzi na kusema kuwa uchaguzi huo “ulikwenda kinyume na kanuni za msingi za kidemokrasia.”

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#