Dollar

0,0000

%

Euro

0,0000

%

Gram Gold

0,0000

%

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Paul Biya, Rais mkongwe zaidi duniani, mwenye umri wa miaka 92 ameapishwa kuwa Rais wa Cameroon kwa muhula wa nane.

Paul Biya, Rais mkongwe zaidi duniani, aapishwa Cameroon

Paul Biya wa Cameroon, ambaye ndiye Rais mwenye umri mkubwa zaidi duniani, ameapishwa kwa muhula wa nane kuwa Rais wa nchi hiyo siku ya Alhamisi, baada ya uchaguzi wenye utata uliochochea maandamano.

Katika hotuba yake ya kuapishwa, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 92 ameahidi kurejesha utulivu katika taifa hilo la Afrika ya Kati na kuwalaumu wanasiasa wasio na uwajibikaji pamoja na raia wanoishi nje ya nchi kwa kuchochea vurugu.

“Napochukua madaraka, natambua kwa kina uzito wa hali ambayo nchi yetu inapitia. Natambua wingi na ukali wa changamoto tunazokabiliana nazo. Natambua kina cha hali ya kukata tamaa na ukubwa wa matarajio ya wananchi,” Biya aliwaambia waliokuwa wakimsikiliza.

Kulingana na taarifa kutoka vyanzo viwili vya Umoja wa Mataifa, vikosi vya usalama viliwaua raia 48 wakati wa maandamano dhidi ya kuchaguliwa tena kwa Biya. Serikali haijatoa taarifa wala kutoa makadirio yake kuhusu idadi ya waliouawa au kujeruhiwa katika machafuko hayo.

Matokeo rasmi yalionyesha kuwa Biya alipata ushindi mkubwa kwa kupata asilimia 53.66 ya kura dhidi ya mpinzani wake Issa Tchiroma Bakary, aliyepata asilimia 35.19. Aidha muhula huu mpya unaweza kumuweka madarakani hadi atakapokaribia miaka 100.

Tchiroma alijitangaza mshindi muda mfupi baada ya uchaguzi wa Oktoba 12, na maandamano yakazuka katika maeneo mbalimbali baada ya matokeo ya awali kuonyesha Biya, ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1982, akiongoza katika uchaguzi huo.

Tchiroma, ambaye hapo awali alikuwa msemaji wa serikali na alijiuzulu wadhifa wake wa uwaziri mwezi Juni, alisema wiki iliyopita kuwa wanajeshi waliokuwa waaminifu kwake walimsindikiza hadi eneo salama, jambo lililoashiria uwezekano wa mgawanyiko ndani ya jeshi.

Hata hivyo, hakufafanua ni askari wangapi waliokuwa wamehusika.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#