Sport
Dollar
42,2010
0.2 %Euro
48,8636
0.16 %Gram Gold
5.404,2000
0.28 %Quarter Gold
9.158,9600
0 %Silver
65,2700
0.37 %Mwili wa Mollel ulikuwa ni sehemu ya miili mingine 22 iliyorudishwa kutoka kwa makubaliano ya kusitisha vita vya Gaza, yaliyofikiwa Oktoba 10.
Israel imesema kuwa kikundi cha Hamas kimerejesha mabaki ya aliyekuwa mwanafunzi wa Kitanzania, Joshua Loitu Mollel.
Mollel ambaye alikuwa anasomea kilimo nchini Israel, alichukuliwa kinguvu na kuuwawa wakati wa shambulio la Oktoba 7 katika eneo Kibbutz Nahal Oz.
Kikundi cha Hamas kinadaiwa kurudisha mwili wa Mollel siku ya Jumatano Novemba 5, 2025 ikiwa ni baada ya siku 761, kama sehemu ya mpango wa usitishwaji vita vya Gaza, ambao uliratibiwa na Rais Donald Trump wa Marekani.
"Baada ya kukamilika kwa shughuli ya utambuzi... wizara ya mambo ya nje imeijulisha familia ya mateka huyo kuwa mwili wa mpendwa wao umerejeshwa," Ofisi ya Waziri Mkuu ilisema.
Taarifa hizo, pia zilithibitishwa na jeshi la Israel.
Mwili wa Mollel ulikuwa ni sehemu ya miili mingine 22 iliyorudishwa kutoka kwa makubaliano ya kusitisha vita vya Gaza, yaliyofikiwa Oktoba 10.
Kama sehemu ya mpango huo, Hamas ilikuwa ikiwashikilia mateka 48 mjini Gaza, huku 20 wakiwa hai na wengine 28 wakiwa wamekufa.
Comments
No comments Yet
Comment