Dollar

0,0000

%

Euro

0,0000

%

Gram Gold

0,0000

%

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Siku ya Alhamisi, mahakama hiyo ilimkuta Kony na hatia ya makosa mbalimbali, ikiwemo mauaji, ubakaji na utesaji.

Mahakama ya ICC yathibitisha mashitaka dhidi ya Joseph Kony wa Uganda

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ya mjini The Hague imethibitisha makosa 39 ya kivita na uhalifu wa kibinadamu dhidi ya Joseph Kony wa Uganda.

Siku ya Alhamisi, mahakama hiyo ilimkuta Kony na hatia ya makosa mbalimbali, ikiwemo mauaji, ubakaji na utesaji.

Kiongozi huyo wa kikundi cha Lord's Resistance Army (LRA) anadaiwa kuendesha udhalimu humo kaskazini mwa Uganda kati ya Julai 2002 na Disemba 2005.

Kulingana na taratibu za mahakama ya ICC, kesi huanzwa kusikilizwa mara baada ya uthibitisho wa mashitaka.

Hata hivyo, mahakama hiyo yenye makao makuu yake mjini The Hague nchini Uholanzi, hairuhusu kusikilizwa kwa kesi bila uwepo wa mshitakiwa mahakamani.

Mara ya mwisho kwa Kony kuonekana hadharani ilikuwa ni mwaka 2006.

Kulingana na majaji wanaoshughulikia kesi hiyo, kuna kila msingi wa kuamini kuwa Kony alikuwa akihusika na makosa hayo 39.

Makosa hayo ni pamoja mashambulizi ya LRA dhidi ya shule na kambi za watu waliokosa makazi, utesaji wa watu, ndoa za kulazimisha, ubakaji na kadhalika.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#