Sport
Dollar
42,1498
0.06 %Euro
48,5703
0.24 %Gram Gold
5.388,7500
-0.06 %Quarter Gold
9.055,1100
0 %Silver
65,0500
-0.16 %Gharama hiyo ni sawa na ile iliyokuwa ikitumika kwa kipindi cha kuishia Oktoba 31, 2025.
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) nchini Tanzania imetangaza bei ya kikomo kwa bidhaa za mafuta kwa Tanzania Bara zitakazotumika kuanzia Novemba 5, 2025.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo, watumiaji wa vyombo vya petroli wataendelea kulipia Dola 1.14 kwa lita (sawa na Shilingi 2,752 za Kitanzania).
Gharama hiyo ni sawa na ile iliyokuwa ikitumika kwa kipindi cha kuishia Oktoba 31, 2025.
Kwa upande mwingine, watumiaji wa dizeli wataendelea kulipia Dola 1.10 (Shilingi 2,704 za Kitanzania) kwa lita moja ya nishati hiyo kama ilivyokuwa kwa kipindi cha mwezi uliopita.
Aidha, katika taarifa yake, EWURA imewataka wafanyabiashara wote wa bidhaa za mafuta ya petroli kwa rejareja na jumla kuuza mafuta kwa bei zilizotangazwa na mamlaka hiyo na atakayekiuka agizo hilo hatua kali za kisheria zitachukuchuliwa dhidi yake.
Pia, imevitaka vituo vyote vya mafuta kuchapisha bei za bidhaa za mafuta ya petroli katika mabango yanayoonekana bayana yakionesha bei za mafuta, punguzo, vivutio vya kibiashara vinavyotolewa na kituo husika ili pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja waweze kununua bidhaa hizo katika vituo vinavyouza kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani.
Kwa mujibu wa EWURA, kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja ni kosa na adhabu kali itatolewa kwa kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika.
Comments
No comments Yet
Comment