Dollar

0,0000

%

Euro

0,0000

%

Gram Gold

0,0000

%

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Rais wa Kenya William Ruto atoa wito wa kuachiliwa kwa Wakenya wanaoshikiliwa nchini Ukraine baada ya kufanya maongezi ya simu na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

Rais Ruto atoa wito wa kuachiliwa kwa Wakenya wanaoshikiliwa Ukraine

Rais wa Kenya, William Ruto ametoa wito wa kuachiliwa kwa Wakenya wanaoripotiwa kushikiliwa nchini Ukraine, kufuatia taarifa kwamba baadhi ya vijana wa Kenya walihusishwa kinyume cha sheria katika vita vinavyoendelea kati ya Urusi na Ukraine.

Katika mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, Rais Ruto alieleza wasiwasi wake kuhusu hali ya Wakenya ambao huenda walidanganywa au kulazimishwa kujiunga na mapigano hayo. Alisema viongozi hao wawili wamekubaliana kuongeza uelewa kuhusu hatari za mikakati ya ulaghai inayolenga vijana wasiojua kinachoendelea.

“Nimemuomba Rais Zelensky kusaidia kuachiliwa kwa Mkenya yeyote anayeshikiliwa nchini Ukraine. Namshukuru Mheshimiwa Rais kwa kukubali ombi langu hilo,” alisema Rais Ruto.

Rais Ruto pia alimpongeza Rais Zelensky kwa maandalizi ya Ukraine Food Summit itakayofanyika mwishoni mwa mwezi huu, na akaeleza dhamira ya Kenya kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.

Katika taarifa iliyotolewa kutoka mjini Kyiv, Rais Zelensky alithibitisha mazungumzo hayo na kusema kuwa alimjulisha Rais Ruto kuhusu mashambulizi yanayoendelea ya Urusi dhidi ya raia na miundombinu ya Ukraine. Alionyesha shukrani kwa Kenya kwa kuunga mkono juhudi na msimamo wa Ukraine.

 “Tulijadili pia suala la Urusi kuajiri raia wa kigeni kushiriki katika vita vyake haramu. Tunafahamu mbinu za udanganyifu zinazotumika, na tutaendelea kushirikiana na Kenya ili kukomesha vitendo hivyo,” alisema Rais Zelensky. 

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#