Dollar

42,3350

0.2 %

Euro

49,1712

0.05 %

Gram Gold

5.547,4900

-0.07 %

Quarter Gold

9.430,0100

0 %

Silver

69,2000

0.51 %

Uwezo wa Tanzania kupata mikopo kutoka taasisi za kimataifa huenda ukakumbana na changamoto baada ya sifa yake kuharibika kimataifa, amesema Rais Samia Suluhu Hassan siku ya Jumanne wakati wa kuwaapisha mawaziri.

Tanzania huenda ikakabiliwa na changamoto kupata mikopo kutoka nje, amesema Rais Samia

Rais Samia, mwenye umri wa miaka 65, ambaye alitangazwa mshindi kwa asilimia 98 ya kura katika uchaguzi wa Oktoba uliogubikwa na machafuko kati ya raia na vikosi vya usalama, hakufafanua kilichosababisha kuharibika kwa sifa ya Tanzania.

Makundi ya kutetea haki za binadamu, vyama vya upinzani na Umoja wa Mataifa wamesema kwamba mamia ya watu huenda waliuawa katika machafuko hayo, ingawa serikali inakanusha takwimu hizo na kusema si za kweli.

“Mara nyingi tunategemea kupata kutoka nje: mikopo kutoka taasisi mbalimbali za kimataifa, mabenki ya kimataifa, lakini yaliotokea nchini kwetu yametutia doa kidogo,” alisema Rais Samia.

, kwa hiyo huenda yakatupunguzia sifa ya kupata hiyo mikopo kwa urahisi kama tulivyopata muhula wa kwanza wa awamu hii

“Kwa hiyo huenda yakatupunguzia sifa ya kupata mikopo hiyo kwa urahisi kama tulivyopata katika muhula wetu wa kwanza wa awamu hii… sifa mbaya tuliyojijengea inaweza kuturudisha nyuma.”

Wachunguzi wa Umoja wa Afrika walisema uchaguzi huo haukuwa wa kuaminika na walithibitisha kuwepo kwa uhalifu wa kujazwa masanduku ya kura. Serikali imepinga ukosoaji huo na kusisitiza kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.

 Rais Samia ameahidi kuchunguza vurugu za uchaguzi na wiki iliyopita alitoa rambirambi kwa familia zilizopoteza wapendwa wao, na hivyo kuwa tamko lake la wazi zaidi kuhusu machafuko hayo ambayo yamesababisha mgogoro mkubwa zaidi wa kisiasa nchini kwa miongo kadhaa.

Wakati wa kuwaapisha mawaziri katika mji mkuu wa Dodoma siku ya Jumanne, aliwasisitiza viongozi kuelekeza nguvu zaidi katika kukusanya mapato kutoka vyanzo vya ndani.

Mwezi Juni, wizara ya fedha ilisema inapanga kukopa kiasi cha shilingi trilioni 8.7 kutoka nje katika mwaka wa fedha 2025/26 (Julai–Juni). Katika bajeti yake ya 2024/25, serikali iliweka makadirio ya kupata ruzuku na mikopo nafuu ya nje yenye thamani ya shilingi trilioni 5.13.

 

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#