Dollar

42,3350

0.2 %

Euro

49,1712

0.05 %

Gram Gold

5.547,4900

-0.07 %

Quarter Gold

9.430,0100

0 %

Silver

69,2000

0.51 %

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemteua binti yake, Wanu Hafidh Ameir, kuwa Naibu Waziri wa Elimu. Hafidh Ameir, mwenye umri wa miaka 43, ni Mbunge wa Jimbo la Makunduchi.

Rais wa Tanzania amteua binti na mkwe wake katika Baraza la Mawaziri

Alifanikiwa kutetea nafasi yake katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Wakati huohuo, Rais Suluhu Hassan amemteua Mohamed Mchengerwa, mume wa Hafidh Ameir, kuwa Waziri wa Afya. Mchengerwa, mwenye umri wa miaka 46, ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji.

Mtoto wa Rais wa zamani apewa nafasi serikalini

Mtoto wa Rais wa zamani wa Tanzania, Jakaya Kikwete, naye anaonekana katika orodha ya wajumbe wapya wa serikali, Ridhwani Kikwete, ameteuliwa kuwa waziri katika Ofisi ya Rais.

Atakuwa anasimamia Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Ridhwani, mwenye umri wa miaka 46, pia ni Mbunge wa CCM anayewakilisha Jimbo la Chalinze.

Katika mabadiliko hayo ya serikali, Rais Suluhu Hassan – aliyeshinda uchaguzi wa Oktoba 29 kwa karibu asilimia 98 ya kura – ametangaza baraza jipya lenye mawaziri 27 na manaibu waziri 29.

Waliopigwa kalamu

Viongozi saba waandamizi waliokuwa kwenye baraza la mawaziri la awali wamekosa nafasi katika baraza hilo jipya. Miongoni mwao ni aliyekuwa Waziri wa Nishati, Doto Biteko, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, na Waziri wa Biashara, Seleman Jafo.

Katika serikali mpya:

Khamis Musa Omar ataongoza Wizara ya Fedha.

Mahmoud Thabit Kombo ameendelea kushika nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje.

Prof. Riziki Shemdoe atakuwa Waziri wa Elimu, akisaidiwa na naibu wake mpya, Wanu Hafidh Ameir.

Daniel Chongolo ataongoza wizara ya kilimo.

Judith Kapinga atakuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#