Sport
Dollar
42,3350
0.2 %Euro
49,1712
0.05 %Gram Gold
5.547,4900
-0.07 %Quarter Gold
9.430,0100
0 %Silver
69,2000
0.51 %Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Jumatatu alimteua balozi wa nchi hiyo nchini China, Khamis Mussa Omar, kuwa waziri wa fedha katika baraza lake jipya la mawaziri kufuatia uchaguzi uliokumbwa na utata mwezi uliopita.
Katika hotuba yake ya moja kwa moja, Rais Samia amesema Anthony Mavunde ataendela kuwa waziri wa madini na Mahmoud Thabit Kombo kuendelea kuwa waziri wa mambo ya nje.
Wiki iliyopita, Hassan alimchagua aliyekuwa waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba, kuwa waziri mkuu.
Rais Samia alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais kwa asilmia 98 katika uchaguzi wa Oktoba, lakini zoezi hilo lilikumbwa na maandamano ya kupinga shughuli za uchaguzi.
Makundi ya kutetea haki za binadamu na vyama vya upinzani yanasema mamia ya watu waliuawa katika machafuko hayo, ingawa serikali inapingana na takwimu hizo.
Rais Samia ameahidi kuchunguza vurugu za uchaguzi na siku ya Ijumaa alitoa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao, ikiwa ni mara yake ya kwanza kuzungumza hadharani kuhusu machafuko hayo, ambayo yamesababisha mgogoro mkubwa wa kisiasa nchini humo katika kipindi cha miongo kadhaa.
Comments
No comments Yet
Comment