Sport
Dollar
42,3350
0.2 %Euro
49,1712
0.05 %Gram Gold
5.547,4900
-0.07 %Quarter Gold
9.430,0100
0 %Silver
69,2000
0.51 %Taifa hilo limeshuhua kuapishwa kwa baraza jipya la mawaziri, Novemba 18 huku kukiwa na maingizo mapya katika baraza hilo lenye jumla ya wizara 27.
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaapisha mawaziri na manaibu mawaziri wapya watakaokuwa sehemu ya baraza lake la mawaziri ndani ya serikali ya awamu ya sita.
Shughuli hiyo ya uapisho, inakuja siku moja baada ya Rais Samia kulitangaza Baraza jipya la Mawaziri, katika Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma.
Baraza hilo, ambalo lina jumla ya wizara 27, mbili zikiwa mpya, limeshudia baadhi ya waliokuwa mawaziri na manaibu wawiri wakiwekwa kando, huku kukiwa kuna maingizo mapya.

Waliowekwa kando
Kati ya walioshindwa kupita kwenye uteuzi huu, ni pamoja na aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko, aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Damas Ndumbaro, Hussein Bashe (Kilimo) na Pindi Chana (Maliasili na Utalii).
Wengine ni Innocent Bashungwa (Mambo ya Ndani), Jenista Mhagama (Afya) Seleman Jafo (Viwanda na Biashara).

Sura ngeni
Mbali na waliowekwa kando, zipo sura ambazo zinaingia kwenye baraza hili kwa mara ya kwanza.
Kwa mfano, katika baraza hili kutakuwepo na Paul Makonda, ambaye ni mbunge wa Jimbo la Arusha mjini.
Katika baraza hili, mwanasiasa huyo machachari, atahudumu kama Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo.
Yupo pia binti wa Rais Samia, Wanu Hafidh Ameir ambaye atakuwa Naibu Waziri wa Elimu.
Wengine ni Daniel Chongolo(Waziri wa Kilimo), Bashiru Ally (Waziri wa Mifugo na Uvuvi), Joel Nanauka( Waziri wa Maendeleo ya Vijana), pamoja na Ngwaru Maghembe na James Ole Millya, ambao kwa watahudumu kama manaibu waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Comments
No comments Yet
Comment