Dollar

0,0000

%

Euro

0,0000

%

Gram Gold

0,0000

%

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

ACT-Wazalendo imesisitiza kuwa, ni kosa la jinai kuharibu ushahidi wakati kuna shauri la kisheria linaloendelea.

Tanzania: Chama cha ACT-Wazalendo chalaani uchomwaji wa nyaraka za Uchaguzi wa Zanzibar

Chama cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania, kimelaani mpango wa tume ya Uchaguzi wa Zanzibar (ZEC) wa kuchoma na kuteketeza nyaraka za Uchaguzi wa Oktoba 2025, uliofanyika visiwani humo.

Katika taarifa yake iliyotolewa Februari 4, 2026, chama hicho kimedai kuwa, kwa muda wa wiki mbili, kuanzia Januari 21, maombi ya chama hicho kisheria, ya kuiomba Mahakama itoe Amri kwa Tume ya Uchaguzi kuleta Mahkamani Nyaraka muhimu za uchaguzi kutokana na umuhimu wa nyaraka hizo katika kuamua Kesi zilizowasilishwa, yamekwama katika Ofisi ya Msajili wa Mahakama Kuu bila sababu za msingi.

“Baada ya tangazo la jana, sasa tumefahamu kwamba kumbe kuchelewa huku si kwa bahati mbaya; ni mkakati wa makusudi wa "kupunguza kasi ya utafutaji haki" ili kuipa nafasi ZEC kuchoma ushahidi wa kile kilichotokea kwenye vituo vya kupigia na kuhesabu kura,” kilidai chama hicho kupitia taarifa yake.

ACT-Wazalendo imesisitiza kuwa, ni kosa la jinai kuharibu ushahidi wakati kuna shauri la kisheria linaloendelea. 

Kwa mujibu wa ACT-Wazalendo, kuteketeza nyaraka hizo, si utaratibu wa kisheria, bali uhujumu wa ushahidi na dharau ya wazi kwa masuala yaliyoko Mahakamani na kufanya maamuzi kwa nia ovu.

Februari 3, 2026, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, iliidhinisha zoezi la kuharibu (kuteketeza) nyaraka zote zilizotumika katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa mwaka 2025 baada ya kukamilika kwa muda wa siku 90 tangu kumalizika kwa Uchaguzi huo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na tume hiyo, zoezi la kuteketeza nyaraka hizo linafanyika kwa mujibu wa kifungu cha 98(3) cha Sheria ya Uchaguzi namba 4 ya mwaka 2018, ambacho kinaitaka Tume ya Uchaguzi kuharibu nyaraka zote zinazohusiana na Uchaguzi Mkuu baada ya kupita siku 90 tangu kukamilika kwa Uchaguzi huo.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#