Dollar

39,1011

0.04 %

Euro

44,4609

0.52 %

Gram Gold

4.202,2600

1.92 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Siasa za jiografia za kimataifa zinaendeshwa kwa gharama ya bara Afrika; mamlaka za kimataifa zenye ushawishi hazitoi umakini mzuri kwa matamanio ya bara hili..

Siku ya Afrika: Mwenyekiti wa Tume ya AU atoa wito nchi zote za Afrika kujiinua ili kuinua Afrika

Wakati maadhimisho ya Siku ya Afrika yakifanyika jijini Addis Ababa, wito umetolewa kwa nchi wanachama wa AU kujichukulia jukumu la nchi binafsi kujiinua ili kijumla Afrika iinuke pamoja.

Haya yamesemwa na mwenyekiti wa Tume ya AU, Mahmoud Ali Youssouf katika hotuba yake kwa Umoja wakati wa maadhimisho.

‘‘Hakuna shaka kwamba uwezo wa Afrika, rasilimali za madini, ardhi ya kilimo na uwezo wa viwanda unapaswa kuzingatiwa,’’ alisema Mohammud.

Pia aliongeza kuwa ni jukumu la kila Amuafrika kulinda rasilimali kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Alisema kuwa siasa za jiografia za kimataifa zinaendeshwa kwa gharama ya bara Afrika; mamlaka za kimataifa zenye ushawishi hazitoi umakini mzuri kwa matamanio ya bara hili.

‘‘Ni jukumu la msingi la nchi wanachama wetu kuunda thamani inaowezekana katika bara kupitia mchakato wa kubadilisha thamani,’’ aliongeza Mahmoud.

Mahmoud alisisitiza haja ya kuimarisha na kukuza soko huru ya Afrika ili kulinda biashara kwa misingi ya kuheshimiana na wanachama, na kujenga uchumi wa Afrika.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#