Sport
Dollar
39,1011
0.04 %Euro
44,4609
0.52 %Gram Gold
4.202,2600
1.92 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Tundu Lissu amechaguliwa katika nafasi ya mojawapo ya Makamu Wenyeviti wa Muungano huo wa Kisiasa duniani wenye lengo la kupigania sera za kisiasa za vyama vya mrengo wa kulia, akiwa bado anazuiliwa gerezani Tanzania.
Kiongozi wa chama cha upinzani Tanzania Tundu Lissu amechaguliwa bila kuwepo kama mmoja wa manaibu wenyekiti wa muungano wa huo wa Demokrasia Duniani IDU.
CHADEMA ilithibitisha kuwa mwenyekiti wake Lissu ameteuliwa bila kupingwa na yeyote baada ya kuhitimisha msururu wa mikutano huko mjini Brussels Ubelgiji.
‘‘Rekodi ya Mh. Tundu Lissu ya kutotetereka katika kupigania haki, utawala bora na demokrasia nchini Tanzania licha ya mazingira magumu yakiwemo ya jaribio la kuuawa ilimfanya aaminiwe na wajumbe kutoka nchi mbalimbali duniani.’’ ilisema sehemu ya taarifa ya CHADEMA mtandaoni.
Malengo ya vyama vya kihafidhina
Katika uchaguzi wa uongozi mpya wa Muungano huo, wajumbe walimchagua pia Waziri Mkuu wa zamani wa Canada Stephen J Harper kama mwenyekiti kwa muda wa miaka mitatu.
Kuchaguliwa kwa Tundu Lissu kumekuja wakati anazuiliwa gerezani kuuhusiana na kesi zinazomkabili za uhaini na kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni, kesi ambazo amedai kuwa zimechochewa kisiasa.
Ikiwa na makao yake makuu nchini Ujerumani, IDU ina wanachama 84 kamili na washirika kutoka nchi 65.
IDU huruhusu vyama vya siasa vya kihafidhina vya "kati-kulia" kote ulimwenguni kuanzisha mawasiliano na kujadili maoni tofauti kuhusu sera ya umma na masuala yanayohusiana.
Wanachama wa Kudumu
Lengo lao lililotajwa ni kukuza "demokrasia na sera za haki za vyama vya mrengo wa kati kote ulimwenguni"
IDU ilianzishwa mjini London tarehe 24 Juni 1983 wakati huo ikiwa na wanachama asili 19.
Afrika ina wanachama 8 wa kudumu katika muungano huo zikiwemo, Kenya, Tanzania, Nigeria, Uganda, Morocco, Afrika Kusini, Ivory Coast na Ghana.
Comments
No comments Yet
Comment