Dollar

40,3884

-0.01 %

Euro

47,2741

0.47 %

Gram Gold

4.409,3900

1.35 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Hii inafuatia makubaliano ya amani kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kikundi chenye silaha cha M23 Movement (AFC/M23).

Shirika la Msalaba Mwekundu lasema liko tayari kuwasaidia waliokuwa wamezuiliwa na M23

Umoja wa Mataifa umekaribisha hatua ya kutiwa saini kwa azimio la Kanuni kati ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kikundi cha silaha AFC/M23.

“Umoja wa Mataifa bado umejitolea kuunga mkono juhudi za amani, ulinzi wa raia na utulivu nchini DRC kwa ushirikiano wa karibu na mamlaka za kitaifa, washirika wa kikanda na kimataifa,” amesema Katibu Mkuu wa UN Antonio Gutteres.

Julai 19, 2025, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kundi la waasi la M23 waliahidi kutia saini makubaliano ya amani ifikapo Agosti 18, katika sherehe zilizofanyika mjini Doha nchini Qatar.

Hii walisema ilikuwa ni ishara ya maendeleo hata licha ya kutokamilika kwa maelezo yanayohitajika kujadiliwa.

Wawakilishi wa pande zote mbili walitia saini tamko la kanuni zinazoweka ratiba hiyo mpya, katika hafla iliyofuata miezi ya upatanishi wa Qatar baada ya mazungumzo kuanza Aprili.

Wakati huo Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) imesema iko tayari kusaidia au kuwezesha kuachiliwa kwa watu waliozuiliwa kuhusiana na mzozo nchini DRC.

Hii inafuatia makubaliano ya amani kati ya DRC na kikundi chenye silaha cha M23 Movement (AFC/M23).

Tangu mwaka 2025 kikundi hicho kimethibiti maeneo ya kaskazini mwa DRC huku ikiwakamata wananchi na kutishia usalama nchini humo.

"Timu yetu nchini DRC itasaidia kuwezesha kuachiliwa kwa wafungwa wa pande zote mbili ili waweze kurudishwa nyumbani salama na kuunganishwa na familia zao," alisema rais wa ICRC Mirjana Spoljaric.

"Mipango ya kibinadamu kama vile kuachiliwa kwa wafungwa mara nyingi ni hatua za kwanza ambazo zinaweza kujenga imani na uaminifu kati ya wahusika katika njia ndefu ya amani."

Kati ya tarehe 30 Aprili na 15 Mei, ICRC ilisaidia kuwasafirisha zaidi ya wanajeshi 1,300 waliopokonywa silaha na familia zao kutoka Goma hadi Kinshasa.

Operesheni hiyo, iliyokua takriban kilomita 2,000 katika eneo la vita, ilitekelezwa kwa ombi la Wizara ya Ulinzi na maveterani wa DRC, MONUSCO, na vuguvugu la Congo Alliance River/M23 kwa ICRC kufanya kazi kama mpatanishi asiyeegemea upande wowote wa kibinadamu.

"Mgogoro wa kikatili mashariki mwa DRC umenasa vizazi vya raia katika mzunguko wa miongo mingi ya mateso, vifo na kuhama makazi yao," alisema Rais Spoljaric.

"Tamko hili lililopatanishwa na Qatar, pamoja na makubaliano yaliyotiwa saini kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda huko Washington, DC mwezi uliopita, inatoa fursa muhimu kwa kanda hiyo kutayarisha mustakabali mpya unaojikita katika amani na utulivu."

ICRC imefanya kazi nchini DRC tangu 1978, kutoa ulinzi na usaidizi kwa waathiriwa wa migogoro ya silaha.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#