Sport
Dollar
43,4990
0.19 %Euro
51,6240
-0.9 %Gram Gold
6.788,9600
-9.85 %Quarter Gold
12.225,8700
-6.97 %Silver
116,5000
-28.39 %Hatifungani za Sukuk za 2026 kufikia sasa ni zaidi ya dola milioni 580, kiwango kikubwa kikiwa ni cha nchini Benin cha dola milioni 500, kulingana na wataalamu.
Mauzo ya hatifungani za Kiislamu nchini Benin yamehamasisha mataifa ya Afrika kutafakari mfumo wa fedha wa misingi ya sharia, baada ya kudhihirika kwa uwezo wake katika uwekezaji, washauri na wachanganuzi wamesema.
Rothschild's Gatien Bon, ambaye alikuwa mshauri wa taifa hilo la Afrika Magharibi kuhusu mauzo yake ya hatifungani kimataifa, ameeleza mfumo wa sukuk kama "mabadiliko makubwa" kwa nchi huru za Afrika katika ukopaji.
"Hii inatoa fursa ya uwekezaji katika maeneo mbalimbali kimsingi na kimfumo barani Afrika," amesema Bon.
Benin, ambayo iliuza hatifungani za miaka saba za sukuk pamoja na kufungua tena hatifungani za dola 2038, imepata maombi ya dola zaidi ya bilioni 7, ikiwa ni zaidi ya kiwango kilichotolewa cha hatifungani hizo.
Mikakati
"Tumeona nchi nyingi zikija kwetu kutuuliza kuhusu mikakati…kujaribu kuelewa vizuri vile mfumo huu unafanya kazi na wadau gani walioko kwenye soko," amesema Nicole Kearse, mkuu wa fedha katika shirika la African Legal Support Facility (ALSF).
Sukuk imekuwa "eneo linalofuatiliwa zaidi", Kearse -- ambaye shirika lake liko chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika, ambayo hushauri serikali kuhusu masuala kama soko la mitaji -- alisema mapema wiki hii.
Bashar Al-Natoor, mkuu wa idara ya mfumo wa Kiislam katika shirika la Fitch Ratings, anasema hatifungani za sukuk Afrika zimepanda hadi dola bilioni 3 mwaka 2025, kutoka dola milioni 112 million mwaka uliotangulia, zaidi ikiwa ni kutokana na kurudi kwa kiwangoi cha Misri cha dola bilioni 2.8 baada ya kutokuwepo kwa mwaka mzima. Kwa kulinganisha, mauzo ya hatifungani za kimataifa Afrika yamezidi dola bilioni 13 kwa nchini Nigeria, Afrika Kusini, na Kenya.
Hatifungani za Sukuk za 2026 zimezidi dola milioni 580, hasaa kutokana na dola milioni 500 za Benin ambao walikuwa wanauza kwa mara kwanza, Al-Natoor amesema.
Nigeria, ambayo imeuza hatifungani za sukuk kwa sarafu za nchi hiyo, ni miongoni mwa nchi ambazo zinaangazia uwezekano wa kuwa na mfumo wa fedha wa Kiislam unaotumia sarafu ya dola, huku Rais Bola Tinubu akitaka bunge liidhinishe mauzo ya hatifungani za sukuk kimataifa.
Senegal pia imesema inaangalia uwezekano wa masoko ya kitaifa na kimataifa ya sukuk.
Admassu Tadesse, rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo, anasema kutakuwa na faida kubwa kwa serikali kupata uwekezaji kutoka kwa mataifa ya Ghuba.
"Kuna hamu sana kwa wawekezaji kutoka mataifa ya Ghuba kuwekeza katika masoko yanayoibuka, hasa barani Afrika," Tadesse alisema wakati wa majadiliano katika kikao.
Comments
No comments Yet
Comment