Dollar

0,0000

%

Euro

0,0000

%

Gram Gold

0,0000

%

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Mkuu wa Majeshi nchini Uganda, Muhoozi Kainerugaba aiomba radhi Marekani kufuatia 'tweets' zake za awali.

Mkuu wa Majeshi wa Uganda aiomba radhi Marekani

Mkuu wa Majeshi wa Uganda Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ameiomba radhi serikali ya Marekani, baada yeye mwenyewe, kuweka jumbe tata, kwenye mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter), ambazo baadaye alizifuta.

Katika jumbe hizo, Muhoozi alidai kuwa Ubalozi wa Marekani wa jijini Kampala, ulikuwa unahusishwa na siasa za upinzani nchini humo, na hata kutangaza kusitishwa kwa ushirikiano wa kijeshi kati ya Uganda na Marekani.

Kauli hizo zilizua taharuki na wasiwasi wa kidiplomasia.

Jenerali Muhoozi ambaye pia ni mwana wa Rais wa Uganda alieleza kuwa amezungumza na Balozi wa Marekani nchini Uganda na kuthibitisha kuwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili bado uko sawa.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#