Sport
Dollar
43,4990
0.19 %Euro
51,6240
-0.9 %Gram Gold
6.788,9600
-9.85 %Quarter Gold
12.225,8700
-6.97 %Silver
116,5000
-28.39 %Inafuatia uamuzi wa Afrika Kusini kumfukuza Balozi mdogo wa Israel, na kuzidisha mvutano wa kidiplomasia unaohusiana na kesi ya mauaji ya halaiki ya Gaza
Siku ya Ijumaa Israel ilimfukuza balozi wa Afrika Kusini huko Palestina, Shaun Byneveldt, na kumtaka aondoke ndani ya muda wa saa 72, katika kulipiza hatua ya Afrika Kusini kumfukuza balozi mdogo wa Israel.
Wizara ya mambo ya nje ya Afrika Kusini imesema Shaun Byneveldt ni balozi wao kwa Taifa la Palestina lakini ameidhinishwa kupitia Israel, kulingana na taarifa.
“Shaun Byneveldt ni balozi wa Taifa la Palestina wala siyo Israel, mpango wa Israel wa kuingilia masuala mengine inafanya mabalozi wa taifa hilo waidhinishwe kupitia wao. Hii inadhihirisha hatua ya Israel kukataa kutambuliwa kimataifa kwa taifa la Palestina,” alisema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini Chrispin Phiri katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa X.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel imesema kuwa uamuzi wa kumfukuza mwanadiplomasia huyo wa Afrika Kusini ulitolewa na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na Waziri wa Mambo ya Nje Gideon Saar.
Ilieleza kile walichokiita “shutuma za uongo” za Afrika Kusini dhidi ya Israel katika majukwaa ya kimataifa na “hatua zisizo na msingi” zilochukuliwa dhidi ya balozi mdogo wa Israel.
“Mwakilishi mwandamizi wa kidiplomasia wa Afrika Kusini, … Shaun Edward Byneveldt, hatakiwi kuwepo hapa nchini na lazima aondoke Israel ndani ya saa 72,” wizara ilisema kupitia taarifa, ikiongeza kuwa “hatua zaidi zitachukuliwa katika kipindi kifaacho.”
Balozi wa Israel kufukuzwa
Mapema siku ya Ijumaa, Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini ilitangaza kuwa kaimu balozi wa Israel nchini Afrika Kusini, Ariel Seidman, amefukuzwa nchini humo kutokana “na mfululizo wa ukiukwaji wa taratibu za kidiplomasia ambazo ni changamoto kwa uhuru wa Afrika Kusini,” ikiwemo kile kinachoonekana kama kumtukana Rais Cyril Ramaphosa.
Afrika Kusini pia ilimtaka Seidman kuondoka nchini katika kipindi cha saa 72.
Seidman amekuwa balozi mdogo wa Israel tangu Novemba 2023, wakati Israel ilipomrejesha nyumbani balozi wao nyumbani baada ya Afrika Kusini kuwaondoa wanadiplomasia wao nchini Israel kutokana na vita vya mauaji ya halaiki vya nchi hiyo huko Gaza.
Comments
No comments Yet
Comment