Sport
Dollar
0,0000
%Euro
0,0000
%Gram Gold
0,0000
%Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Afrika Kusini imetangaza kuwa mjumbe wa Israel Ariel Seidman, ni mtu asiyekaribishwa nchini humo, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo siku ya Ijumaa.
Serikali ya Afrika Kusini imemshutumu Balozi Mdogo wa Israel Seidman kwa ukiukaji wa taratibu na maadili ya kidiplomasia, ikisema kuwa vitendo hivyo vinatishia moja kwa moja mamlaka na uhuru wa Afrika Kusini.
"Ukiukwaji huu unajumuisha matusi ya mara kwa mara dhidi ya Rais Cyril Ramaphosa kupitia mitandao rasmi ya kijamii ya Israel na kutoifahamisha DIRCO (Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini) kuhusu ziara zinazodaiwa kufanywa na maafisa wakuu wa Israel," wizara hiyo ilisema.
Wizara imesema Seidman anatakiwa kuondoka Afrika Kusini ndani ya saa 72, kulingana na taarifa iliyowekwa kwenye tovuti yao rasmi.
Ubalozi wa Israel mjini Pretoria haukutoa ufafanuzi kuhusu hatua hiyo.
Kesi ya Afrika Kusini katika Mahakama ya ICJ
Ujumbe wa kidiplomasia wa Israel mjini Pretoria haukutoa ufafanuzi kuhusu hatua hiyo.
Mahusiano ya kidiplomasia kati ya Afrika Kusini na Israel yamezorota kufuatia kesi ya Afrika Kusini katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), ikiiandama Israel kwa madai ya mauaji ya halaiki kuhusiana na vita vyake dhidi ya Gaza.
Israel imekataa vikali madai hayo, ikisema kuwa hayana msingi.
Comments
No comments Yet
Comment