Dollar

38,7438

0.29 %

Euro

43,5658

-0.07 %

Gram Gold

4.115,9500

0.29 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Baadhi ya raia wa Tanzania wanaodaiwa faini ya bili za maji, wamepata afuweni baada ya rais Samia Suluhu Hassan kutangaza kuwafutia mzigo huo wadaiwa.

Rais wa Tanzania amewafutia rasmi faini za madeni ya bili za maji raia wake

Baadhi ya raia wa Tanzania wanaodaiwa faili ya bili za maji, wamepata afuweni baada ya rais Samia Suluhu Hassan kutangaza kuwafutia mzigo huo wadaiwa.

Madeni hayo ni yale yanayohusiana na Mamlaka za Maji nchini humo.

Tangazo la msamaha huo, limetolewa katika Bunge la nchi hiyo Alhamisi na Waziri wa Maji Juma Aweso, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

"Rais Samia amesamehe faini zote za huduma ya maji. Tunataka wateja wanaohusika kwenda katika Mamlaka za Maji katika maeneo yao kurudisha huduma zao za maji,"  amesema Waziri Aweso na kuongeza kuwa, tarehe ya mwisho ya msamaha huo ni Mei 31, 2025.

Waziri Aweso amesema kuwa hata wateja ambao huduma ya maji ilisitishwa baada ya kushindwa kulipa, wanahusika na msamaha huo.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#