Dollar

38,7338

0.28 %

Euro

43,6102

-0.02 %

Gram Gold

4.121,3100

0.42 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Kuanzia Oktoba 2024, Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii (SHA) umechukua nafasi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambao umekuwepo tangu 1966.

Kenya yasajili wafungwa katika huduma mpya ya bima ya taifa ya afya

Serikali imezindua mpango wa kusajili wafungwa katika Mamlaka ya Taifa ya Afya ya Jamii (SHA). Hii ni huduma mpya ya bima ya afya ya kitaifa ambayo serikali ya Rais William Ruto imezundua.

Zoezi hili litafanywa kote nchini katika magereza na vituo vyote vya uangalizi, kwa nia ya kutomuacha mtu yeyote nyuma - Huduma ya Afya kwa Wote.

Serikali italipa ada hizo kwa wafungwa kupitia Idara ya Huduma za Urekebishaji.

Harakati ya usajili, ambayo pia inajumuisha Kitambulisho cha Kitaifa, ilizinduliwa katika Gereza la Wanawake la Lang’ata jijini Nairobi.

Waliokuwepo ni Makatibu Wakuu Dkt Ouma Oluga (Huduma za Kimatibabu) na Belio Kipsang (Huduma za Uhamiaji na Raia).

Dkt Salome Beacco anayesimamia huduma za Urekebishaji, alisema ni muhimu kwa kila Mkenya kujisajili katika mfumo wa SHA ili mtu yeyote asibaki nyuma.

"Wakati mwingine tunapinga mabadiliko kwa sababu hatuelewi," alisema.

Aliongeza kuwa katika magereza, wafungwa 8,000 tayari wamesajiliwa, na mpango huo sasa unaongezwa ili kuhakikisha kila mfungwa anapata huduma hiyo.

Kwa nini umekuwa ukipingwa?

Kuanzia Oktoba 2024, Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii (SHA) umechukua nafasi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambao umekuwepo tangu 1966.

Huduma hii mpya ya SHA imekuwa ikipingwa na wakenya kadhaa ambao wanadai hakukuwa na haja ya kufanyika ka mabadiliko.

Kwa wanaotegemea mshahara, chini ya bima hii mpya kiwango cha mchango wa kila mwezi ni 2.75% ya mshahara wa jumla na ni lazima waajiri wachangie kiasi hiki kufikia tarehe 9 mwezi unaofuata.

Kwa wale wasio na mishahara basi chini ya mfumo huu mpya wa afya kila Kaya itatoa mchango wa kila mwaka kwa kiwango cha 2.75% ya jumla ya mapato yake, na mchango wa chini wa shilingi za kenya 300 kwa mwezi na hakuna malipo ya juu ya kila mwaka. Hili lazima liwasilishwe siku 14 kabla ya tarehe ya mwisho ya mchango wa kila mwaka.

Viongozi wengi na wataalamu wa afya, wakiwemo maafisa wa kliniki, wametoa wasiwasi wao hadharani, huku wengine wakihisi kutengwa na hazina hiyo.

Maafisa hao sasa wanatakiwa kujisajili kwenye mfumo mpya watakaopewa kandarasi, huku Wakenya wengi wakiwa bado hawaelewi kikamilifu ni manufaa gani watapata.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#