Sport
Dollar
38,7482
0.27 %Euro
43,5829
-0.1 %Gram Gold
4.127,4300
0.57 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Rais wa Kenya William amemteua Erastus Edung Ethekon kuwa mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi nchini humo.
Rais wa Kenya William Ruto amemteua Erastus Edung Ethekon kuwa mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini humo (IEBC).
Kwa sasa, IEBC, ambayo inatakiwa kuwa na makamishna sita na mwenyekiti, haina kamishna hata mmoja kwenye tume, kwa kuwa waliokuwepo wamestaafu, kujiuzulu au kuondolewa ofisini kutokana na madai ya kwenda kinyume na kanuni.
Ethekon anamrithi Wafuka Chebukati, ambaye alikuwa amekamilisha muda wake wa miaka sita, baada ya kuwepo uongozini kuanzia Januari 2017 hadi Januari 2023. Chebukati alifariki dunia kutokana na mshtuko wa moyo katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi akiwa na umri wa miaka 63 mwezi Februari 2025.
Makamishna wanachaguliwa kwa muhula mmoja tu wa miaka sita na baada ya hapo hawaruhusiwi kuwa tena makamishna wa tume ya uchaguzi.
Wateule kuidhinishwa na bunge
Rais Ruto pia amemteua Ann Njeri Nderitu, Moses Alutalala Mukhwana, Mary Karen Sorobit, Hassan Noor Hassan, Francis Odhiambo Aduol na Fahima Araphat Abdallah kuwa makamishna.
Ofisi ya rais imesema siku ya Alhamisi kuwa kamati ya kusaili makamishna wa IEBC ilipendekeza majina mawili kwa nafasi ya mwenyekiti, na majina tisa kwa ajili ya uteuzi wa makamishna.
Kutoka katika majina hayo rais alitakiwa kuchaguwa makamishna saba, ikiwa ni pamoja na mwenyekiti.
Rais Ruto amewasilisha majina hayo bungeni ili bunge liweze kujadili na kuidhinisha.
Mara nyingi tume ya uchaguzi ya Kenya, IEBC, imekuwa ikilaumiwa kwa namna inavyosimamia uchaguzi mkuu, kukiwa na madai ya upendeleo dhidi yao.
Upinzani iliwasilisha kesi dhidi ya IEBC
Kwa mfano, katika uchaguzi wa Agosti 2022, upinzani, ukiongozwa na mgombea wao wa urais Raila Odinga, ulishtumu baadhi ya makamishna wa IEBC, ikiwemo aliyekuwa mwenyekiti wakati huo Chebukati, kwa kuchakachuwa kura ili kumpa ushindi Ruto.
Tume ya IEBC imekanusha madai hayo, na Odinga akashindwa kesi mahakamani, ambapo alitaka matokeo ya uchaguzi wa urais yabatilishwe.
Comments
No comments Yet
Comment